Friday, June 10, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dr Magufuli amewaapisha majaji aliowateua hivi karibuni ambao ni Jaji Kiongozi Lila na Fedinand Wambari leo Ikulu jijini Dar es salaam;https://youtu.be/sRL88RdCw7s

SIMU.TV: Serikali imetakiwa kuangalia upya maamuzi ya kuweka kodi ya ongezeko la thamani asilimia 18% katika sekta ya utalii; https://youtu.be/4b77B9x6DFM

SIMU.TV: Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imekabidhi hundi ya shilingi milioni 50 kwa mkuu wa mkoa wa Dar Makonda kusaidia madawati; https://youtu.be/PzW6sLHtEIQ

SIMU.TV: Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari nchini vimetakiwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya migogoro ya ardhi inayozidi kusumbua amani ya nchi;https://youtu.be/MQMTYGULzfc

SIMU.TV: Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kukisoma vizuri kitabu cha Quran katika mwezi huu wa ramadhani;https://youtu.be/gxPP76cbTLQ

SIMU.TV: Wananchi wametakiwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inayojengwa katika maeneo inakuwa bora ili iweze kuwa endelevu; https://youtu.be/-1lb-LFyNjI

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewakamata vijana 711 wanaojihusisha na vitendo mbalimbali vya kihalifu; https://youtu.be/7Z6OZwnK7_o

SIMU.TV: Bei ya sukari mkoani Ruvuma imezidi kupanda bei kutoka shilingi 2800 hadi 3500 katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani; https://youtu.be/eiVXyk9vG_o

SIMU.TV: Taasisi ya utoaji mikopo ya Bayport imewataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua viwanja na nyumba kupitia taasisi hiyo; https://youtu.be/sKBtw2uWuGg

SIMU.TV: Madereva Bodaboda mkoani Iringa waombwa kuongeza ubunifu ili kuweza kuifanya kazi hiyo kama fursa inayoweza kubadili maisha yao;https://youtu.be/7jKAc_gb2rY

SIMU.TV: Wagombea mbalimbali wa uchaguzi katika klabu ya Yanga waendelea kujinadi kwa wanachama wao ili kuweza kuchaguliwa katika uchaguzi wa klabu hiyo hapo kesho;https://youtu.be/wIqSSWS9DZs

SIMU.TV: Mbio za kimataifa za Kilimanjaro marathon zinatarajia kufanyika tarehe 24 August mkoani Kilimanjaro huku kukiwa na kauli mbiu ya utunzaji wa mazingira;https://youtu.be/QWptNVwQLPU

SIMU.TV: Maelfu ya watu wahudhuria sala ya kiislamu katika maombolezo ya kumuaga aliyekuwa bingwa wa ndondi duniani marehemu Mohammed Alli;https://youtu.be/Sg7LgshgzPU

SIMU.TV: Wakazi wa kitongoji cha Mkongo njalamatata katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuingilia mgogoro wa ardhi kati yao na kanisa katoliki la Liganga. https://youtu.be/kPolPS5licI   

SIMU.TV: Waziri wa ardi nyumba na maendeleo ya makazi amerejesha shamba la ekari 9025 kutoka kwa mwekezaji katika wilaya ya Ulanga. https://youtu.be/jSlQPlp3pGA
SIMU.TV: Mpango wa madiwani wa halmashauri wa wilaya ya Kilolo wa kumsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri umeshindwa kutokana na kutofuata utaratibu.https://youtu.be/IogUzDhi1f4

SIMU.TV: Serikali imeaaswa kuweka mikakati thabiti katika kufanikisha mpango wa maendeleo iliojiwekea katika mwaka wa fedha unaoanza. https://youtu.be/9zeS3xVLOyY
SIMU.TV: Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Augustine Mahige ametoa wito kwa watanzania kukemea mauaji yanayotokea nchini.https://youtu.be/XRB8Q5HG99Y
SIMU.TV: Mkoa wa Mbeya umetekeleza agizo la rais la utengenezaji wa madawati kwa asilimia 95 katika wilaya zote za mkoa huo. https://youtu.be/43s9vcxsGEY

SIMU.TV: Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imetoa kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ununuzi wa madawati katika mkoa wa Dar es Salaam.https://youtu.be/9Ucf2Lk5LFU

SIMU.TV: Bodi ya wakuu wa vyombo vya utangazaji vya umma katika eneo la nchi za SADC wamekubaliana kuanzisha chombo cha habari kitakacho shirikisha nchi za SADC.https://youtu.be/TZCpEBVUAF0

SIMU.TV: Mfumuko wa bei kwa mwezi mei umeongezeka kidogo ukilinganisha na mwezi Aprili na hii ni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula. https://youtu.be/yqC6dE9sigo

SIMU.TV: Wataalamu wa masuala ya uchumi wameishauri serikali kutoongeza vyanzo vya mapato badala yake isimamie mamlaka ya mapato nchini kukusanya kodi kwa ufanisi.https://youtu.be/09ErM8y9mdc

SIMU.TV: Wafanyabiasha wa soko la Darajani Unguja wamesema kupanda bei kwa bidhaa za vyakula msimu huu wa mfungo hauepukiki kutokana na uwepo wa wanunuzi wengi kuliko upataikanaji wa bidhaa. https://youtu.be/iwni6e8o9C4

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Mbeya ameiomba serikali kutumia bidhaa zinazotengenewa na Jeshi la magereza nchini ili kuliinua jeshi hilo kiuchumi. https://youtu.be/S83PICtuhVo

SIMU.TV: Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Yanga imesema kuwa maandalizi ya uchaguzi huo yameenda vizuri. https://youtu.be/_WNcugiOW2A

SIMU.TV: Kocha wa makipa wa klabu ya Yanga amesema amewaandaa vyema makipa wake kuelekea michuano ya shirikisho. https://youtu.be/aj5BUSr3xXc

SIMU.TV: Jumla ya wanafunzi 70 mkoani Mtwara wamechaguliwa kwenda mkoani Mwanza kwa ajili ya michezo ya UMISETA . https://youtu.be/lTwXJ3dhXyQ

No comments: