Friday, June 10, 2016

KUWA MJASILIAMALI NA TAJIRIKA NA UFUGAJI WA KUKU KUPITIA INCUBATORKatika miaka ya hivi karibuni ufugaji wa kuku umekua kwa kiasi kikubwa na kuwa mtaji mkuu wa wajasiriamali wadogo na wakubwa katika kujiingizia kipato.

Mkurugenzi wa Kuku Project Mary David
Hata hivyo ufugaji wa kuku nao umekuwa ukienda kwa wakati kutokana na ukuaji wa teknolojia. Moja ya teknolojia hizo ni mashine za kutotoleshea vifaranga kitaalamu; ‘incubator’.

Mary David maarufu kama ‘Mama Kuku’ ni Mkurugenzi wa Kuku Project Tanzania, ambaye pia ni msambazaji wa mashine za kisasa za Incubator, yeye anasema kuwa mashine hizo zimekuwa mkombozi kwa wafugaji wa kuku nchini kwa kuwa huuzwa kwa bei rahisi inayoendana na mahitaji ya mfugaji mwenyewe.


“Incubator zetu ni za bei tofauti kuanzia shilingi laki nne na nusu ambazo zina uwezo wa kubeba mayai arobaini na nane na kubwa kabisa ambayo hubeba mayai elfu kumi na tisa mia saba kumi na mbili ambayo huuzwa kwa shilingi milioni ishirini,” anasema Bi. Mary.

Mbali na hayo, Bi. Mary anasema kuwa incubator hizo huwa na uwezo wa kutumia umeme, nishati ya jua na pia kuhifadhi umeme kwa masaa sita baada ya umeme  kukatika ambapo pia mtumiaji atapata fursa ya kuelekezwa jinsi ya utumiaji wake huku mashine hizo zikiwa na waranti ya mwaka mzima.
Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kununua Incubator fika DAR ES SALAAM,MAGOMENI MWEMBE CHAI,NYUMA YA KANISA LA  WASABATO. SIMU : +255 653 691 138+255 715 908 307,+255 678 226 988

Kujua zaidi Like Page yao kwa kubofya hapa :


No comments: