Friday, June 10, 2016

WAZIRI PROF. MBARAWA AKEMEA HUJUMA KWENYE MIUNDOMBINU YA BARABARA MKOANI SINGIDA

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bw. Gishuli Charles (wa nne kushoto), wakati alipoanza ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu katika Mkoa wa Singida. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu, na wa tatu kushoto ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo.
 Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa uharibifu wa barabara unaotokana na ajali za barabarani katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilometa 89.3 mkoani Singida.
 Wananchi wa Itigi wakimsilikiza Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, (hayupo pichani) alipotangaza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mkiwa-Itigi-Makongorosi kwa kiwango cha lami itakayoanza kujengwa kwa kilomita 35 mkoani Singida.
 Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo (wa tano kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto) kuhusu mradi wa ujenzi wa mzani katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya ambao ujenzi utakamilika hivi karibuni.
 Muonekano wa ujenzi wa kituo cha Mzani Itigi, kinachojengwa katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, mkoani Singida.
 Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akionesha moja ya picha ya uharibifu wa alama za barabarani uliofanywa na wananchi katika ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3.
 Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akihutubia wananchi wa Itigi mara baada ya kukagua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 mkoani Singida, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 98.
 Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisalimiana na wananchi wa Itigi mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara. Katikati ni Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Omary Yahya Massare.

Muonekano wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 inayojengwa na Mkandarasi SynoHydro Corporation Limited kutoka China inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 109 mkoani Singida.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments: