Thursday, June 23, 2016

RC MAKALLA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU WA GEPF JIJINI MBEYA LEO

 Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (katikati) akiwa tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, Joyce Shaidi na Kulia kwake ni Mkurugeni Mkuu wa Mfuko huo, Daud Msangi. wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Osward Urassa (kulia) na Mjumbe wa Bodi hiyo, Ahmed Kilima.  Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni "Hifadhi ya Jamii kwa Kila Kaya".
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Daud Msangi, akitoa hotuba yake ya ufunguzi iliyoambatana na taarifa fupi ya Mfuko huo, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF),  Joyce Shaidi akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kutoa hotuba yake.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016.  Katika Hotuba yake, Mkuu wa Mkoa amesema Serikali itaendelea kuwahimiza Wananchi wenye uwezo wa kuingiza kipato, kujiunga na Mifuko ya Jamii, kwani mifuko hii inawezesha wanachama kujijenga wakati wanazalisha kipato na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujiunga na Mifuko ya Hifadhi za Jamii.
 Sehemu ya Wakurugenzi wa Mifuko mingine ya Hifadhi za Jamii, wakiwa kwenye Mkutano huo. Toka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Crescentius Magor, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga, Pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu.
Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya GEPF pamoja wa Wadau wengine wa Mfuko huo, wakishitiki Mkutano huo.
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo kutoka Taasisi mbalimbali nchini.
Washiriki toka maeneo mbalimbali wakifatilia kwa makini Mkutano huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016.
Mkutano ukiendelea.
Wakifatilia Mkutano kwa Umakini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Daud Msangi (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, Osward Urassa (kulia) wakisikiliza jambo kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko huo, Aloyce Ntukamazina.
Tuzo kwa Washindi wa Uchangiaji kwa Wakati.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini, Eliud Sanga ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa LAPF, akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya umoja huo.
MC Mwakipesile akiendesha Mkutano huo.

Mkurugenzi wa Masoko na Uendeshaji wa Mfuko wa Malipo ya Kustaafu wa GEPF, Anselini Peter akitoa taarifa fupi ya Mpango mpya wa Bodaboda (Bodaboda Scheme) uliozinduliwa rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), unaofanyika leo Juni 23, 2016, katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF),  Joyce Shaidi wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mpango mpya wa Bodaboda (Bodaboda Scheme), leo Juni 23, 2016 katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akimpongeza mmoja wa waendesha Bodaboda Mkoa wa Mbeya ambayo ni wanachama wa Mfuko wa GEPF kwa kuwa wanachama wapya katika Mpango huo.
Mwendesha Bodaboda huyo akiijaribu pikipiki.
Picha ya Pamoja na Baadhi wa Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii.
Picha ya Pamoja na Wanachama wapya wa GEPF katika Mpango wa Bodaboda.
Picha ya Pamoja wa Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali zilizoshiriki Mkutano huo.


Picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Mfuko wa GEPF.


No comments: