Monday, April 18, 2016

Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaongozwa na Askofu Josephat Gwajima wachangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye mahitaji

Na Neema Mwangomo
 Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima leo wamejitokeza kwa wingi kuchangia damu  ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Katika shughuli hiyo ya utoaji damu MNH kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Kanda ya Mashariki wamefanikiwa kukusanya chupa nyingi za damu.
Akizungumzia shughuli hiyo Ofisa Uhamasishaji wa Damu salama wa MNH, Hamisi Kubiga amesema kwamba mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa kwani kwa siku chupa zinazotakiwa kukusanywa ni 70 hadi 100 ili kuweza kukidhi mahitaji ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Kubiga amesema kuwa baadhi ya makundi ambayo yanauhitaji mkubwa wa damu ni kina mama wajawazito, majeruhi, na wagonjwa wa saratani hivyo amewaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
“Hivi sasa tunaendesha mpango wa uchangiaji damu, tunashukuru wapo wananchi wamejitokeza lakini bado tunawaomba wananchi, taasisi kampuni binafsi na umma waje kwa wingi ili kwa pamoja tuwasaidie wenzetu wenye uhitaji,” amesema Kubiga.
Shughuli ya utoaji damu inaendelea jumapili ijayo kwenye kanisa hilo la Ufufu na Uzima.
Endapo taasisi, kanisa, shule na makundi mengine yanataka kuchangia damu. Wawasiliane na Mkuu wa Idara ya Maabara wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa namba 0754 575 981, Mkuu wa Idara ya Maabara namba0713 777 595 na Ofisa Uhamasishaji wa Damu salama wa hospitali hiyo namba 0754 597 165.   
 Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaongozwa na Askofu Josephat Gwajima wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye mahitaji ya damu. Shughuli hiyo imefanywa leo na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
 Mshauri wa MN, Erica Ishengoma akiandika maelezo baada ya kumsikiliza mmoja wa waumini wa kanisa hilo, huku wengine wakiwa kwenye foleni kabla ya kutoa damu.

 Ofisa Uhamasishaji wa uchangiaji damu salama, Hamisi Kubiga (kulia) na Erica Ishengoma wakiwapatia chupa maalumu za kuweka damu baada ya kupima uzito.

 Damu ikitolewa
  Mtaalamu wa maabara Anthony wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akiendelea na shughuli ya utoaji damu leo katika kanisa hilo.
Wataalamu wa maabara, Peter Onesmo (kulia) na Anthony (wa pili kulia) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiendelea kutoa damu baada ya waumini hao kujitokeza kwa wingi leo katika kanisa hilo lilipo Ubungo jijini Dar es Salaama.
 Muumini wa kanisa hilo, Vedasto Aloysi akitolewa damu leo katika kanisa hilo na mtaalamu wa maabaram Peter Onesmo.

 Damu iliyotolewa na waumini wa kanisa hilo 
 Hawa Hamisi (18) akichangia damu leo. Hawa amesema kuwa anasikia fahari kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali hiyo.



Waumini wa Askofu Gwajima Watia Fora Utoaji Damu Muhimbili
 Waumini wa kanisa hilo wakiendelea kujitolea kutoa damu leo Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Waumini wa kanisa hilo wakiendelea kutoa damu leo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea kutoa damu leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

No comments: