Wajumbe wa kamati ya kudumu
ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii wakipitia taarifa ya shirika la
utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe
pwani na maendeleo yake.
Mkurugenzi wa shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha taarifa ya shirika hilo kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe
Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape
Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati
hiyo Bw.Peter Serukamba.Picha na Daudi Manongi-Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea
mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo
kisarawe Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu
ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati
kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu
ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya kudumu
ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Bw.Peter Serukamba katika viwanja vya
urushaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Kisarawe
No comments:
Post a Comment