Meneja
Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses
akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vyenye matundu 14,
vitakavyohudumia wanafunzi 850 katika shule ya Msingi ya Makambi, Songea
Mkoa wa Ruvuma, ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 4.7 kulia ni
Meneja wa Oparesheni wa tawi la Songea, Simon Mlelwa.
Wanafuzni wakishangilia kupata vyoo
Noves akibadilishana mawazo na baadhi ya walimu na wazazi
Sehemuya vyoo hivyo
Wanafunzi wa shule ya
msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifurahia vyoo vya
kisasa vilivyojengwa na Benki ya Posta Tanzania.
Na Mwandishi wetu, Songea
BENKI ya posta Tanzania, TPB, imekabidhi vyoo vyenye
thamani ya shilingi milioni 4.7 kwa shule ya msingi Makambi iliyoko Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma.
Akikabidhi vyoo hivyo vyenye matundu 14 vilivyojengwa
na benki hiyo ili kusaidia kuondokana na upungufu wa vyoo kwenye shule hiyo
mwishoni mwa wiki, Meneja mahusiano na mawasiliano wa TPB, Noves Moses, alisema
msaada huu wa benki ni sehemu ya mchango kwa jamii
katika kuboresha miundombinu ya shule na hivyo kufikia lengo la kutoa elimu bora
hapa nchini.
Kwa kutambua juhudi za Rais za kutoa elimu bure kwa
wanafunzi kote nchini, ambapo kumekuwepo na ongezeko kubwa sana la wanafunzi,
benki ya posta inayofuraha kuunga mkono juhudi za Mh.Rais na msaada huu wa vyoo
utasaidia kuweka mazingira bora ya utoaji elimu lakini pia mahudhurio ya
wanafunzi, alisema Noves.
Alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wadau wa elimu
kulichukulia suala la elimu bure kama
kigezo cha kutokuchangia sekta hiyo na baadala yake wanadai ni kazi ya serikali
pekee jambo ambalo siyo sahihi katika uboreshaji elimu.
“Suala la elimu bure lisiwe kigezo cha wadau kushindwa
kuichangia sekta hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea baadhi ya shule kushindwa
kuwa na mazingira mazuri ya watoto kujisomea pamoja na walimu wao kutokuwa na
morali ya kufundisha” alisema Meneja huyo wa
mahusiano na mawasiliano.
Noves alisema kuwa Benki ya Posta Tanzania inafanya kazi kwa kiwango kikubwa na
serikali hivyo imetoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa upande wa afya na
elimu huku katika upande wa elimu wamechangia madawati na ujenzi wa vyoo bora
vya kisasa kwenye shule mbalimbali hapa nchini .
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu
msaidizi wa shule hiyo, Kanisius Ngongi awali akitoa
taarifa ya shule hiyo kabla ya kukabidhiwa vyoo hivyo alisema kuwa shule hiyo
ina wanafunzi 850 na matundu ya vyoo yapo 14 na kuwa vyoo
vyote vina maji ya kutosha.
Ngongi aliipongeza benki
hiyo alisema kuwa shule hiyo kwa sasa imeshabadilika, mazingira yamekuwa bora kwa upande wa vyoo vya
wanafunzi ambavyo kwa sasa hakuna shule ndani ya Manispaa hiyo yenye vyoo kama
hivyo.
Mwalimu Ngongi alisema kuwa licha ya vyoo vya
wanafunzi kuwa bora lakini bado kuna changamoto ya
vyoo vya walimu maana vyoo walivyokuwa wakivitumia vimeshapoteza ubora wake na
kuwafanya walimu hao kupata shida mahala pa kujisitili hivyo amewaomba wadau
mbalimbali waweze kuchangia kama Benki ya Posta inavyojitolea.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vyenye matundu 14, vitakavyohudumia wanafunzi 850 katika shule ya Msingi ya Makambi, Songea Mkoa wa Ruvuma, ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 4.7 kulia ni Meneja wa Oparesheni wa tawi la Songea, Simon Mlelwa.
No comments:
Post a Comment