Tuesday, January 5, 2016

SIMU TV HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Watu 4 wamefariki dunia na wengine 35 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Luwinzo na Lori la mizigo mkoani Iringa;https://youtu.be/08GzJ9yetes   

Zoezi la kewekea alama ya X kwa nyumba zilizoko mabondeni laendelea hii leo huku likisimamiwa na askari wa FFU zaidi ya elfu moja.https://youtu.be/Tehr_QgHnOo  

Mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF wawaonya watoa huduma za afya watakao bainika kugushi au kutoa taarifa za uongo kwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria. https://youtu.be/sUdQx_kFJLw  

Wakazi wa eneo la Keko walalamikia baadhi ya watendaji wa serikali za mitaa kwa kushindwa kutimiza majukumu yao na kupelekea kukwama kwa zoezi la usafi katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam.https://youtu.be/wlThwEU5Edw  

Mamlaka za mikoa nchini zatakiwa kusimamia utekelezaji wa agizo la serikali la kuzuia uuzwaji holela wa chakula usiozingatia usafi hali inayopelekea kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu katika maeneno mbalimbali.https://youtu.be/C3Vghkka_yU  
  
Waziri mkuu Kassim Majaliwa aagiza magunia ya kuhifadhia mahindi yawafikie moja kwa moja wakulima badala ya mawakala huku wale watakaobainika kuhujumu jasho la wakulima kukiona. https://youtu.be/xqtu1KOv_JA  

Hospitali ya taifa ya Muhimbili yapata mashine mpya ya kisasa ya CT SCAN yenye uwezo mkubwa wa kupima wagonjwa. https://youtu.be/CUMHBmzcf28  

Kampuni moja ya uchimbaji wa madini iliyopo wilayani Geita yapewa siku 14 kuanza shughuli za uchimbaji kabla ya kufutiwa lesseni ya uchimbaji.https://youtu.be/vYJscdAPyC0  

Sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 yaendelea kupigiwa kelele na wadau mbalimbali nchini huku ikitajwa kuwa moja ya kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. https://youtu.be/sFdhzeOUTqI

Serikali yaweka mikakati thabiti ya kudhibiti udanganyifu uliokuwa ukifanywa kwenye taasisi mbalimbali za umma kwa kuweka mifumo mipya ya ukaguzi.https://youtu.be/1tSnvtnGaWE  

Halmashauri ya manispaa ya Ilala yaeleza bayana kushindwa kutimiza malengo ya kukusanya bilioni 15 kama kodi ya majengo na badala yake kukusanya shilingi bilioni 1.9. https://youtu.be/1A3l76oO-XI  

Watu 8 wamefariki dunia wakiwemo 4 wa familia moja ya askari polisi Gerald Ryoba ambaye ni msaidizi  wa mkuu wa jeshi la polisi;https://youtu.be/sMrT2rrO05o  

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi  mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam kujadili mustakabali wa taifa;https://youtu.be/5AtfWLI3ZMc   

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakala wa hifadhi ya chakula kanda ya kusini kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali kwa lengo la kuwasaidia wakulima; https://youtu.be/qaH9yZoKaj8  

Zaidi ya familia 50 mkoani Mtwara zimeiomba serikali na jamii kwa ujumla kuwasaidia kufuatia nyumba zao kubomolewa na mvua;https://youtu.be/tcgW3kWHXu4  

Wanafunzi wawili kutoka shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro wanatarajia  kushiriki maonyesho ya kimataifa ya sayansi na teknolojia;https://youtu.be/7HVuWbc_KC8  

Shirikisho la soka nchini TFF limesema lipo njia panda juu ya nani litampigia kura kuwa Rais wa shirikisho la mpira duniani FIFA;https://youtu.be/jXRZEP2UQ3c  

Mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha ya ardhi inatarajia kutoa hukumu tarehe 5 juu ya kesi ya kupinga zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/KJ0impRMYY8

Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi, Mhe.Mwigulu Nchemba aisimamisha bodi ya NARCO kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma;https://youtu.be/qHW868-sr0k  

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dkt. Abdallah Posi amesema serikali haina bodi ya kutoa msamaha wa kodi kwa vifaa vya watu wenye ulemavu; https://youtu.be/B0XtIAZoOuE  

Watu wawili  wamefumaniwa wakitoka nje ya ndoa jijini Mwanza;https://youtu.be/s6qrjCCeZtA

Soko la hisa la Dar es Salaam DSE limeelezea mafanikio yake ya ukwasi kwa kipindi cha miaka minne; https://youtu.be/5ckupYCvWUk   

Mashabiki wa soka nchini wamelezea malalamiko yao juu ya waamuzi wa michuano ya kombe la mapinduzi yanayoendelea visiwani Zanzibar;https://youtu.be/MS-qGcxk_Pg  

Chama cha soka nchini Ghana GFA kimesema kitamchagua Rais wa FIFA atakayekuwa tayari kulisaidia bara la Afrika; https://youtu.be/a0oZIjwp1Ro

No comments: