Tuesday, January 5, 2016

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WAIPIGA JEKI ZAHANATI YA MWINGIRO GEITA

Maafisa wa kitengo cha  Mahusiano ya Jamii katikamgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, William Chungu (kulia) na Zuwena Senkondo (kushoto) wakikabidhi vifaa vinavyotumika wakati wakujifungulia kwa zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita
Zuwena Senkondo wkikabidhi vifaa vya kujifungulia kwa mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita
Kiongozi wa kitengo cha Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Sara Ezra Teri akikabidhi Video Camera ya kisas kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Thoams Mshilu kwa ajili ya kurekodia tamthiliya zao.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii 
Kanda ya Kaskazini,aliyekuwa mkoani Geita.

Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu umekabidhi seti nane za vifaa vya kutolea huduma kwa akina mama wajawazito wanapojifungua, katika halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita vyenye thamani ya shilingi Milioni Tatu.
Akipokea vifaa hivyo Mratibu wa Huduma ya Baba, Mama na Mtoto wa Halmashauri ya Nyang’wale Mkoani Geita Bi Neema Mhoja amesema, “Tunaushukuru Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama na mtoto kwani awali upungufu wa vifaa hivyo umesababisha Wauguzi Wakunga katika zahanati wilayani humo kutoa huduma katika mazingira magumu.”

Naye Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, afya za akina mama ni nguzo ya msingi wa maendeleo katika jamii hivyo Mgodi kwa kutumia utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi mwaka huu ulipata maombi ya vifaa hivyo kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Iyenze na Mwasabuka katika kata ya Mwingiro wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita na umeitikia ombi kwa kukabidhi vifaa hivyo kwa mratibu wa huduma za akina mama na watoto wa wilaya ya Nyang’wale.

Wauguzi katika zahanati ya kata Mwingiro wamekabidhiwa vifaa hivyo ili waweze kuvitumia na kuvitunza kwa ajili ya matumizi kwenye zahanati hiyo inayohudumia wakazi wapatao 12,000 wa kata ya Mwingiro.

Muuguzi  Mkunga wa zahanati ya Mwingiro bwa Costantine Matata Bahebe, na Pendo Ntabudyo, na Elizabeth Lameck amesema, “ Sasa itakuwa rah asana ukipata mzazi maana vifaa vinatosha kwani kwa mwezi tunazalisha akina mama kati ya 20 na 25 hivyo kwa vifaa hivi tufanya kazi katika mazingira ya usafi, usalama na utulivu hata pale tutakapopata wazazi nane kwani kila mmoja atakuwa na kifaa chake kuliko kumsubirisha mzazi wakati unapochemsha vifaa baada ya kuvitumia.
Naye Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo amewaasa wakunga katika zahanati ya Mwingiro kutumia na kuvitunza vifaa hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni Tatu.

No comments: