Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa
machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo.Sehemu ya jingo lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya ranchi za Taifa(NARCO)Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma ilivyotekelezwa.Mwigulu
akiwa na jopo la wataalam wakiendelea kutathimini hasara iliyojitokeza
kutokana na ujenzi mbovu wa machinjio ya kisasa hapa Ruvu.Mwigulu
Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani wakisikiliza kwa
makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa
mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd.Bwire.
Sehemu ya jingo ikiwa imetelekezwa bila kuendelezwa kiujenzi.Hii ni sehemu ya ukuta wa jingo hilo ambao umekatika kutokana na kukaa muda mrefu bila kuendelezwa.Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.Mh.Ridhiwani
kikwete Mbunge wa Chalinze akitoa malalamiko yake kwa Waziri.Mwigulu
Nchemba kuhusu kukosekana kwa mahusiano mazuri kati ya wamiliki wa
ranchi na wananchi wanaozunguka ranchi ya Ruvu.Kwa
mbali hili ndio jengo la machinjio ya kisasa lililokuwa linajengwa na
hatimaye kutelekezwa bila kuendelezwa tangu mwaka 2010.Mh:Mwigulu
Nchemba akiteta jambo na viongozi wanaohusika na kulinda baadhi ya
vifaa vilivyonunuliwa kwaajili ya ranchi hiyo ya kisasa.Mh;Mwigulu Nchemba akioneshwa baadhi ya Ng'ombe wanaopatikana kwenye ranchi hiyo.Mwigulu Nchemba akiwa kazini kwenye shamba la Mifugo la Ruvu hii leo.Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu.
Wakati
Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya
Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya uchapa kazi,Mawaziri wake pia
wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za
maendeleo ya Nchi yetu.
Hii
leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na
Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua
ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.
Katika
hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu
Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa
kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa
kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama
ilivyokusidiwa.
Waziri
huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila
kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni
kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa
ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya
kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo
aliamua ifuatavyo.
Kwanza,Mwigulu
Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya
kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi
huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa
inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo
la ranchi ya ruvu.
Pili,Mwigulu
Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa
kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi
kukamilika kwake.
Pia,waziri
huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote
walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo
usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
Mwisho,Nchemba
amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7
wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha
zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Sambamba
na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari
wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya
nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali
ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia
mali hizo na kuziendeleza.
Picha/maelezo na Festo Sanga Jr
No comments:
Post a Comment