Tuesday, January 5, 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA UHAMIAJI, AAGIZA MAKAMPUNI YENYE KUAJIRI WAGENI YACHUNGUZWE

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini.. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake kwa Viongozi Wakuu wa Idara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati aliyevaa tai) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile, na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha),  Piniel Mgonja. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamishna wa Idara ya Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Idara hiyo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (wanne kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji. Naibu Waziri Masauni alifanya ziara ya kikazi katika idara hiyo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo. Hata hivyo, katika hotuba yake, aliiagiza idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini .
 Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

1 comment:

Anonymous said...

Duuu,kwa mwendo huu hatutaweza kufika na hii kasi ya Mh.Rais ya HAPA KAZI TU,sijui kama hawa mawaziri wanaijua vizuri na nini wananchi tutegemee toka kwao.Swala la wageni kufanya kazi si la kutaka uchunguzi ufanywe na hao hao waliohusika na utoaji vibali,kwa kasi ya serekali hii ilitakiwa waziri kumwambia huyo kamishina wa uhamiaji nipatie majina ya wageni wanaofanya kazi kwa vibali,kampuni walizoajiriwa na ni kazi gani wanazofanya.Hapo ndipo angeliweza kuwajua ni wageni gani hawakusitahili kufanya kazi hapa Tanzania,hili la kila siku kuunda vikosi kazi na uchunguzi tunarudi nyuma na kupunguza kasi ya serekali ya awamu ya Tano