Sunday, December 13, 2015

BONANZA LA UZAZI WA MPANGO KWA VIJANA LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay akizugumza na wananchi  (hawapo pichani)  kwenye bonanza la uzazi wa Mpango kwa vijana ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwembeyanga,Temeke jijini Dar.
 Mgeni rasmi Zukrah Mkwizu akizungumuza na wananchi (hawapo pichani) kuhusiana na suala zima la Uzazi wa Mpango,na kusisitiza kuwa uzazi wa mpangp ni silaha imara ambayo vijana wanaweza kuitumia kupangilia maisha yao na kujikinga dhidi ya utoaji mimba usio salama na kulinda ndoto zao dhidi ya mimba zisizotarajiwa.
 Balozi wa vijana wa Marie Stopes , Doreen Benne akifafanua jambo mbele ya wakazi wa mji wa Temeke na viunga vyake waliofika kwenye kwenye Bonanza la Uzazi wa Mpango kwa Vijana lililofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
 Mwanamuziki Barnabas Elias 'Barnaba akionesha umahili wake wa kulitawala jukwaa katika Bonanza la Uzazi wa Mpango kwa Vijana Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam
Sehemu Ya Wananchi Waliofika Katika Bonanza La Uzazi Wa Mpango Kwa Vijana wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye bonanza hilo ndani viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Jijini Dar Es Salaam
 (Picha na Emmanuel Massaka , Globu ya jamii).


 =======  =======  ========
Wanamuziki na Viongozi wa serikari ya Mkoa wanashirikiana na Marie Stppes Tanzania na zaidi ya Vijana 1,000 kutoka vikundi mbalimbali vya vijana kuhamasisha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango, Mwembeyanga, Wilaya ya Temeke Leo.

Akiongea katika mkutano huu, Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay amesema, “Hiki ni kizazi kikubwa zaidi cha vijana katika hisoria ya Tanzania, asilimia 54 ya Watanzania wapo chini ya umri wa Miaka 20. Mafanikio yao yanamaanisha mafanikio ya Tanzania na mategemeo ya uchumi Imara ambao kila mmoja wetu ataufurahia na kunufaika nao. Lakini wakati huo huo, maisha na matarjio ya vijana yanaharibiwa – au wakati mwingine yanaishia pabaya – kutokana na mimba zisizotarajiwa.”

Asilimia 44 ya wanawake Tanzania – karibu nusu yao – hupata ujauzito wafrikiapo umri wa miaka 19. Huu huwa mwisho wa matarajio/ndoto ya kielimu na taaluma au utoaji mimba usio salama, ambao idadi yao inakadiliwa kuwa 1,500 kila mwaka kwa wanawake wanaoishi Tanzania – wengi wao wakiwa vijana wa kike.

“Vijana wa kiume wanaathirika pia” Aliongeza Mr Tambay, “Wengi wao hujikuta wanakuwa kin baba kabla hawajawa Tayari, hivyo hujikuta wanaachana na mipago ya kwenda chuoni au chuo kikuu ili waweze kutafuta fedha kwa ajili ya familia ambayo hawakuitarajia.”

Championi wengine wa upatikanaji wa huduma za Uzazi wa Mpango kwa vijana kwenye tukio hili ni Bambo, Barnaba, Haika, Mwasiti, Nahreel na Queen Darleen. Message inayotolewa ni kuwa,Uzazi wa Mpango ni silaha imara ambayo vijana wanaweza kuitumia kupangilia maisha yao – kujikinga dhidi ya utoaji mimba usio salama na kurinda ndoto zao dhidi ya mimba zisizotarajiwa.

“Leo tunawaambia vijana wachague Maisha mazuri kwa ajili yao” Alielezea Mr Tambay,“Natunawaomba watu wote wenye madaraka – Manesi, Walimu na Viongozi wa serikari – wasiwe vikwazo kwa upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpago kwa vijana badala yake wawaunge mkono na kwawashauri watumie kiuwajibikaji. Napenda kumalizia kwa kusema, nawashukuru vijana wote  waliofika hapa kushirikiana nasi. 

Maria Stopes ipo hapa kwa ajili yenu na kwa ajili ya kwaunga mkono kufanya maamuzi. Kama una ndoto, zilinde na jilinde kwa Uzazi wa Mpango.


No comments: