Tuesday, September 8, 2015

WAWANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA KANSA YA KIZAZI WAPATA FARAJA

 Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kutangaza mfumo ulioshirikisha taasisi za T-MARC Tanzania,Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation ambayo imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road(ORCI). Kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa T-Mark Tanzania,Diana  Kisaka,Kaimu mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya Ocean road, Beatrice Erasto na Meneja mradi wa T-Mark Tanzania,Doris Chalambo.
 Kaimu mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya Ocean road, Beatrice Erasto akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa mkutano wa kutangaza mfumo ulioshirikisha taasisi za T-MARC Tanzania,Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation ambayo imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road(ORCI).katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa T-Mark Tanzania,Diana  Kisaka na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza.
 Wakina mama wanaotibiwa ugonjwa wa kansa ya kizazi katika hospitali ya Ocean road wakifurahia jambo na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza(kulia) baada ya kutangaza mfumo wa kusaidia matibabu kwa kina mama hao  ulioshirikisha taasisi za T-MARC Tanzania,Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation ambayo imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha akina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road(ORCI).
Baadhi ya wageni waalikwa na wakina mama wanaotibiwa ugonjwa wa kansa ya kizazi katika hospitali ya Ocean road, wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliohusu taasisi zisizo za kiserikali za T-MARC Tanzania,Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation  wakitangaza mfumo wa kusaidia matibabu kwa wakina mama hao  ulioshirikisha taasisi hizo   ambapo  Vodacom Foundation imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road(ORCI).

.  Ni kutokana na kuanzishwa kwa huduma ya kuwasaidia
.  Kupitia Vodacom Foundation,T-Marc Tanzania na Pink ribbon red ribbon

Wanawake wanaougua maradhi ya Kansa ya kizazi nchini wamepunguziwa adha ya kusumbuka na gharama za matibabu zinazowakabili.Unafuu huo unatokana na ushirikiano wa taasisi tatu ambazo zimeamua kushirikiana kulivalia njuga tatizo hili ili kuleta unafuu kwa akina mama hususani wenye maisha duni na waishio vijijini.Taasisi hizo ni Vodacom Foundation ,T-MARC Tanzania na taasisi ya kimataifa ya Pink Ribbon Red Ribbon.

Taasisi ya Vodacom imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha akina mama wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam ilipo taasisi ya uchunguzi na matibabu ya Kansa ya Ocean Road (ORCI) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali na kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Msaada huu kwa kuanzia utawalenga akina mama wanaoishi sehemu ambazo taasisi ya Pink Ribbon Red Ribbon inaendesha miradi yake ambayo ni katika mikoa ya Iringa,Mbeya na Mwanza.

Katika ushirikiano huu T-MARC inahusika na kuwapata walengwa kwa ushirikiano na taasisi za afya kwenye mikoa hiyo ambapo baada ya kupatikana wataunganishwa na  mabalozi wa mradi huu kutoka taasisi ya Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT) ambao watapatiwa fedha za kusafirisha walengwa kutoka T-MARC kwa njia ya M-Pesa kwa ajili ya kununua tiketi za usafiri na watakapofika jijijini Dar es Salaam watapokelewa na ufuatiliaji ,gharama za uchunguzi  na gharama za matibabu yao yatafanywa na T-MARC ambayo itahakikisha pia wamalizapo uchunguzi na matibabu wanarejeshwa makwao.Huduma hii pia itatolewa kwa wagonjwa wataopenda kutibiwa katika hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza ambayo itaanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa Kansa katika siku za karibuni.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huu ambao umelenga kuwasaidia wanawake wenye hali ya maisha ya chini uliofanyika leo katika taasisi ya Ocean Road, Meneja wa Miradi wa T-MARC  Doris Chalambo alisema tayari mradi umehudumia akina mama 17 Kutoka mikoa ya Iringa na Mbeya na wanaendelea vizuri kupata matibabu na afya zao zinazidi kuimarika.



Chalambo alisema “Ugonjwa wa Kansa ya kizazi ni tishio hapa nchini na unasababisha vifo vya akina mama wengi na takwimu zinaonyesha  unachukua asilimia 38.4  ukiondoa  wagonjwa wa kansa za aina nyingine.Tanzania pia ni nchi yenye vifo vingi vya Kansa barani Afrika,hivyo lazima tukubali kuwa Kansa hivi sasa ni moja ya magonjwa tishio nchini na unahitaji kuuvaria njuga kwa nguvu zote ili kuutokomeza na kwanusuru wananchi na vifo vinavyotokana na ugonjwa huu”

Aliongeza kusema kuwa Mkoani Mbeya mradi huu  tayari umesaidia akina mama na wanapoelimishwa kujua dalili za ugonjwa wanajitokeza ili wafanyiwe uchunguzi kabla ya ugonjwa kuongezeka na kufikia hatua ya kutotibika na alisema  wengi wameelewa ugonjwa huu na hawaufichi na kuuona kama ugonjwa wa aibu kama ilivyokuwa hapo awali anapotokea mgonjwa anafanya jitihada za kutafuta matibabu haraka.

“Kupitia msaada huu wa Vodacom Foundation na Pink Ribbon Red Ribbon wanawake wote waliojitokeza kuchunguzwa na kukutwa wameisha athirika kwa kiasi kikubwa wanaendelewa kusaidiwa gharama za matibabu”.Alisema Chalambo.

Kwa upande wake Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza amesema kuwa msaada wa Dola za Marekani milioni 87,400 umelenga kusaida matibabu  ya akina mama na kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa kansa ya Kizazi “Tukio hili la leo pia linatupa fursa ya kutoa elimu kwa jamii ya Tanzania kuhusiana na ugonjwa wa Kansa ya Kizazi na nini kifanyike kukabiliana nao kama ambavyo wenzetu wa Pink Ribbon Red Ribbon wameanza kuuvalia njuga kwa ajili ya kuutokomeza hapa nchini”.Alisema

Naye mkuu wa kitengo kinachohusika na ugonjwa wa Kansa ya Kizazi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dk……Kamala amesema kuwa wananchi wengi wameanza kuuelewa ugonjwa huu na wanajitokeza kwa wingi kufanyiwa uchunguzi wanapohisi dalili tofauti na ilivyokuwa katika siku zilizopita.

 “Hivi sasa vipo vituo 130 kwenye mikoa 17 nchini vya uchunguzi wa kansa ya kizazi  na uchunguzi huo na matibabu ni bure na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ina dhamira ya kuhakikisha huduma hizi zinaboreshwa zaidi ila changamoto kubwa imekuwa ni  gharama kubwa za kununua mashine za uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu,tunatoa wito kwa akina mama kuanzia umri wa miaka 30 hadi 50 kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wanapohisi dalili kwa kuwa ugonjwa ukigundulika mapema ni rahisi kutibika na  jambo hili likizingatiwa litaokoa maisha ya  wengi”.Alisema.

No comments: