WANAWAKE wametakiwa kuzimama imara katika
uchaguzi ili kuweza kuchukua nafasi za uongozi katika majimbo ,mikoa, wilaya na
serikalini ili kufikia malengo .
Hayo
yameeelezwa na Mwanaharakati wa masuala ya wanawake Zanzibar Siti Abas Ali wakati
lipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Kwerekwe Wilaya ya Magharibi.
Amesema kuwa kuchukua
nafasi za uongozi kwa wanawake kutasaidia kuweza kujikwamua na hali ya
kimaisha pamoja kuzisaidia familia pindi
zinapofikwa na matitizona kuweza kuyafanyia ufumbuzi.
Siti
aliwataka wanawake wawe makini katika upigaji kura kwa kuwapigia wanawake wenzetu na sio kuwazarau kwani
kufanya hivyo kutawapa moyo na kuweza kufikia pale walipokusudia.
Aidha alifahamisha kuwa jamii iachane na dhana ya kwamba wanawake hawana uwezo wa kuongea kwani kwa wakati
tulionaowanawake wamukuwa na uwezo
mkubwa wa kuongea katika mazingira tofauti.
Nae kwa
upande wake Mwanasheria wa ZAFELA Saada Salum Issa ameitaka jamii wazidishe
mashirikiano ili kuweza kusonga mbele katika harati za kimaisha .
Vile vile
alisema kuwa kwa kiasi fulani wanawake wamepiga hatua kimaendeleo kielimu, kisiasa, na katika.
Sambamba na
hayo amewataka wanawake wasijiweke nyuma na wawe katika harakati za
kijishirikisha katika njacha tofauti za kujikwamua na hali ngumu za kimaisha.
No comments:
Post a Comment