Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe
Balozi
Mulamula aliwahakikishia wnadiaspora waliohudhuria kongamano hilo, kuwa
Serikali ina dhamira ya dhati ya kuwashirikisha Watanzania wanaoishi
ughaibuni ili kuchangia maendeleo ya nchi yao. Hivyo, aliwahimiza kuja
kuwekeza nyumbani kwa kuwa Serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya
uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwapatia ardhi kwa
ajili ya kujenga makazi au kuwekeza.
Aliwaomba
wanadiaspora hao, kuwa mabalozi wazuri wa nchi yao kwa kuzitangaza vema
fursa zinazopatikana nchini katika sekta mbalimbali kama vile kilimo,
miundombinu, nishati, maji, utalii na elimu.
|
No comments:
Post a Comment