Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini
Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na
wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa
kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akimtambulisha
mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba (kushoto)
katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es
Salaam.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba
akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha
urais, Bi. Samia Suluhu katika viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini
Dar es Salaam.
MGOMBEA
mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu amesema awamu ya Serikali ya Tano itakayoundwa na CCM itakuwa
maalum kwa ajili ya ujenzi na ufufuaji wa viwanda nchini ili kuongeza
nafasi ya ajira kwa vijana na kuinua kwa kasi uchumi wa nchi.
Bi. Suluhu ameyasema hayo alipokuwa akiinadi ilani mpya ya Chama Cha
Mapinduzi katika ziara ya kampeni ya jijini Dar es Salaam ya kuinadi
ilani hiyo kwa wananchi juu ya nini Serikali ya CCM itafanya endapo
itapewa ridhaa tena na wananchi kuunda Serikali na kuongoza nchi baada
ya uchaguzi.
Alisema watahakikisha wanajenga viwanda na kuvifufua vile vilivyokufa
ikiwa na lengo la kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na hapo hapo
kuwatambua wafanyabiashara ndogondogo ikiwa ni pamoja na kuwajengea
uwezo katika biashara zao.
"...Tunataka
awamu ya Serikali ya Tano iwe awamu ya viwanda...tunataka asilimia 40
ya ajira ipatikane kwenye sekta ya viwanda...," alisema mgombea mwenza. Mama Anna Abdallah
akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi
ya urais, Jimbo la Kawe kwenye mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye
Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa uchukuzi, Samuel Sitta akizungumza kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Jimbo la Kawe kwenye mkutano
wa kampeni ulofanyika kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini
Dar es Salaam. Burudani yake Isha Mashauzi mara baada ya kusikiliza ilani ya CCM kwenye mkutano huo. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji akichukua taswira ya mkutano huo kwa simu yake kwa ajili ya kumbukumbu.
Alisema
pamoja na hayo Serikali itakayoundwa na CCM itaanzisha dawati maalumu
la bodaboda na bajaji na kukamilisha usajili wa vikundi vyao ili
kuangalia namna ambayo kundi hili la vijana linaweza kufanya shughuli
zao bila kubughuziwa.
Alisema
uimarishaji huo wa madawati ya bodaboda na bajaji utaenda sambamba na
kuongeza mipaka ya kufanyia kazi, kutambua bodaboda na bajaji kwa rangi
kulingana na maeneo zinapofanyia kazi ili zitambulike kwa uraisi.
Alisema
ili kumaliza kero ya foleni na msongamano wa magari jijini Dar es
Salaam, Serikali imepanga kujenga miji mipya maalum na ya kisasa
pembezoni wa jiji hili na kwa kuanzia itajenga mjini huo eneo la Kibaha
ili shughuli nyingine ziwe zikifanyika katika mji huo na Dar es Salaam
kupunguza msongamano, zoezi litakaloenda sambamba na ujenzi wa barabara
ndogondogo za mitaani ambao utapunguza msongamano na foleni katika
barabara kubwa.
Aidha
Bi. Suluhu alisema zitajengwa barabara za juu katika makutano ya
barabara ikiwa pamoja na kuzijenga barabara ndogondogo zikiwemo za Mbezi
Morogoro-Malamba Mawili-Tangi Bovu-Kimara Baruti-Goba na nyinginezo ili
kupunguza msongamano katika barabara kubwa.
Alisema
ili kuboresha huduma za afya jijini Dar es Salaam, Serikali ya CCM
kupitia ilani yake itaiongezea hadhi na kutoa upendeleo kwa Hospitali ya
Mwananyamala ikiwa ni pamoja na kuiongezea watumishi wa kada zote
pamoja na mgao wa dawa kulingana na mahitaji yake. Alisema mbali na hapo
ilani inaeleza watahakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya na
kuhimiza kuwakatia bima wananchi ili waweze kupata huduma hiyo muda wote
bila kujali uwezo wa vipato vyao.
Aliongeza
wafanyabiashara nao hawajasahaulika kwani imetenga maeneo sehemu
mbalimbali ya ujenzi wa masoko kwa wafanyabiashara ndogondogo, ambapo
nafasi takribani 3263 kwa eneo moja zitapatikana na kupewa
wafanyabiashara ndogondogo huku jitihada kama hizo zikiendelea maeneo
mengine.
Kwa upande wa huduma za upatikanaji maji safi na salama zimepewa
kipaumbele pia ambapo mradi mkubwa wa kutoa maji Ruvu Juu na Ruvu Chini
pamoja na ule wa Mto Ng'ombe utamaliza kabisa kero ya maji kwa jiji la
Dar es Salaam baada ya mwaka mmoja ujao.
Mgombea huyo wa urais anaendelea na ziara yake mkoa wa Dar es Salaam kunadi ilani ya CCM.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment