TAREHE 04 – 09 – 2015
UKUMBI WA MIKUTANO WIZARA YA KAZI NA AJIRA
WCF ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kazi na Ajira iliyoundwa
kwa Mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya mwaka
2008 ili kushughulikia masuala ya fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika Sekta ya
Umma na Binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua au kufariki dunia wakiwa
katika utekelezaji wa majukumu ya Mwajiri.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF) umeanzishwa kwa Madhumuni makuu yafuatayo;
·
Kutekeleza matakwa ya Sera ya Taifa ya
Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003 katika kukabiliana na majanga mbalimbali
yanayoikumba jamii ikiwamo ajali, magonjwa au vifo vinavyotokana na kazi;
·
Kutekeleza matakwa ya Kifungu cha 5 cha
Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008;
·
Kulipa fidia stahiki pale mfanyakazi
anapoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi;
·
Kuwasaidia wafanyakazi watakaoumia au kuugua
kutokana na kazi ili waweze kurudi kazini au kushiriki katika shughuli nyingine
zitakazowapatia kipato (ukarabati na ushauri nasaha);
·
Kuweka utaratibu utakaowezesha kuharakisha
malipo ya fidia kwa wafanyakazi au wategemezi wao;
·
Kuweka utaratibu utakaowezesha Mfuko kupokea
michango kutoka kwa waajiri na kufanya malipo;
·
Kukidhi matakwa ya mikataba ya kimataifa
kuhusu fidia kwa wafanyakazi; na
·
Kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa au
vifo katika maeneo ya kazi.
Majukumu ya Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi yatakuwa ni pamoja na;
·
Kusajili waajiri na waajiriwa;
·
kufanya tathmini ya mazingira hatarishi
katika sehemu za kazi;
·
kukusanya michango kutoka kwa waajiri;
·
kuwekeza michango iliyokusanywa;
·
kulipa fidia pale mfanyakazi anapoumia,
kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazofanya;
·
kutunza kumbukumbu za matukio ya ajali,
magonjwa na vifo kutokana na kazi.;
·
kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa au
vifo kutokana na kazi na kuelimisha umma kuhusu kazi za Mfuko.
HAFLA
YA UZINDUZI WA BODI
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Eric Shitindi akitoa hotuba ya utangulizi
juu ya Sheria Na. 20 ya Mwaka 2008 pamoja na uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) kulia kwake ni Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka
Waziri
wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka akitoa hotuba kwa Wajumbe wa Bodi ya
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) pamoja na wageni waalikwa kabla ya
kuzindua Bodi hiyo Rasmi.
Mwenyekiti
wa Bodi Bw. Emmanuel Humba akitoa neno fupi na kueleza namna Bodi ilivyojipanga
kuhakikisha malengo na madhumuni makuu ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi yanafikiwa ikiwa na kuwahakikishia Fidia Stahiki Wafanyakazi Wote.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba akipokea vitendea kazi
pamoja na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008 kutoka kwa Wazi
wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka.
Mwenyelkiti
wa Bodi ya Wadhamini Bw. Emmanuel Humba akipokea chati cha usajili wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi Kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka
(Cheti cha Usajili kimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii Nchini SSRA)
Katibu
Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Eric Shitindi wa pili kushoto, Mhe. Gaudentia
Kabaka wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi
No comments:
Post a Comment