Wednesday, September 9, 2015

TOTAL TANZANIA YADHAMINI MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA SHULE 10 ZA MSINGI JIJINI DAR

 Askali wa usalama barabarani akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya za msingi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa navyeti walivyo tunukiwa mara baada ya kupata mafunzo ya usalama barabarani jijini Dar es Salaam.
 

Na Tom Bishop.
KAMPUNI  ya Mafuta ya Tatal  Tanzania imedhamini mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam.
 
Udhamini wa mafunzo hayo yamegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 20,000 kupeleka kwenye mradi wake wa elimu ya usalama barabarani.
Tatal   imekuwa ikidhamini mafunzo ya Usalama barabarani kila mwaka  kutokana na  kutenga  bajeti hiyo kwa ajili ya mafunzo hayo.
 
Utengaji huo wanatumia Boksi la Usalama barabrani ambao ni mradi wa  kuendelea kwa kipindi cha miaka 10 na utakuwa ukitolewa nchi nzima, kwa maeneo yenye kiwango kikubwa cha hatari za ajali kwa wanafunzi.
 
Mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 150,000 wamefundishwa juu ya usalama barabarani katika jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo.
 
 Boksi la usalama barabarani lina alama za barabarani, maelekezo ya elimu ya usalama barabarani kwa mwanafunzi, maelekezo ya usalama barabarani kwa mwalimu, mfano wa barabara yenye alama na vifaa vingine kama viakisi mwanga, vyeti pamoja na kalamu.
 
Katika mradi huo, mwaka huu Total Tanzania imefanikiwa kuzifikia shule za msingi  10 jijini Dar es Salaam.
 
Shule zilizopata mafunzo hayo ni    Shule ya Msingi Kawe A,Shule ya Msingi Tumaini,Shule ya Msingi Hananasif,Shule ya Msingi Mkunguni, Shule ya Msingi Mwongozo, Shule ya Msingi Yombo Dovya, Shule ya Msingi Jitihada, Shule ya Msingi Mivinjeni , Shule ya Msingi Mzambarauni pamoja na Shule ya Msingi Amani.

No comments: