Mtoto Baraka Dombeni, akiwa na mama yake Bizimana Violet,
akivishwa alama ya utambuzi muda mfupi baada ya kuwasili jana katika kambi ya
wakimbizi ya Nyarugusu, akitokea Wilaya ya Makamba nchini Burundi. Alama hii ni
utambulisho wa kuwawezesha wakimbizi wanaofika katika kambi ya Nyarugusu
kuandikishwa rasmi kabla ya kupewa hifadhi kambini hapo.
Afisa Msajili Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
kuwahudumia wakimbizi (UNHCR), Awadhi Nyanda akichukua taarifa toka kwa familia
mojawapo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaoendelea kuingia nchini kuomba hifadhi. Wakimbizi hawa wanahifadhiwa katika kambi ya
Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kogoma.
Mkimbizi kutoka
Burundi, Sindaye Salvatory akiwa na wenzake, akiwekewa alama yake ya
utambulisho, wakati walipowasili katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu jana,
wakitokea nchini Burundi kuja kuomba hifadhi nchini Tanzania kutokana na hali
ya kisiasa nchini mwao.
Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,
Vivian Vianney akimchukua alama za vidole mkimbizi kutoka nchini Burundi Bw.
Gwasa Jeremia ambaye ni mmojawapo ya raia wa Burundi wanaoendelea kuingia
nchini kuomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma.
Maofisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) wanaohusika na usajili wa wakimbizi wanaopokelewa katika
Kambi ya wakimbizi ya Nyarutgusu, wakiwa katika picha ya pamoja katika Kambi
hiyo iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mwakilishi wa Shirika la OXFAM toka nchini Ireland, Michaelo
Riorpan akisaini kitabu cha wageni alipowasili na wenzake katika kambi ya
wakimbizi ya Nyarugusu jana. Shirika la
OXFAM linatoa misaada mbalimbali kusaidia utoaji wa huduma za maji na utunzaji
wa mazingira katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu. Aliyesimama ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B)
Bw. Fredrick Nisajile ambaye aliupokea ugeni huo.
Mkimbizi kutoka Burundi akipata huduma ya maji katika moja
ya vituo vya maji vilivyojengwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Huduma za maji safi na salama ni mojawapo ya
mambo yanayotiliwa mkazo ili kulinda afya za wakimbizi.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
No comments:
Post a Comment