|
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda (kulia)
akimpokea Mfalme wa Lesotho, Mhe. Letsie III (kulia) alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Mfalme Letsie
ambaye pia ni Kiongozi wa kuhamasisha masuala ya Chakula na Lishe wa
Umoja wa Afrika yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kwanza wa
Dunia kuhusu umuhimu wa kuongeza Virutubisho kwenye Chakula. Mkutano huo
unafanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 11 Septemba, 2015. |
|
Waziri
Mkuu Mhe. Pinda (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi wa TANAPA Dkt.
Allan Kijazi (wa kwanza kulia) kwa Mfalme Letsie (wa kwanza kushoto). |
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (wa kwanza kulia) akimtambulisha aliyekuwa
Mbunge wa Viti Maalumu CCM Arusha Mhe. Catherine Magige (wa pili kutoka
kushoto) kwa Mfalme Letsie (wa pili kutoka kulia).
|
Mfalme Letsie akiwapingia Mkono moja ya vikundi vya ngoma vulivyokuwepo uwanjani hapo |
|
Mhe. Pinda akimwongoza Mfalme Letsie III mara baada ya kumpokea. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Daudi Felix Ntibenda. |
|
Mhe.
Waziri Mkuu kwa pamoja na Mfalme Letsie III wakiwa wameongozana pamoja
na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Ntibenda na Mkurugenzi Msaidizi, Idara
ya Itifaki katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. James Bwana (mwenye tai nyeupe)
Mhe. Pinda akizungumza na Mfalme Letsie mara tuu baada ya kuwasili uwanjani hapo
Picha na Reginald Philip.
TANZANIA
imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Dunia kuhusu umuhimu wa
kuongeza Virutubisho kwenye Chakula kwa ajili ya Lishe Bora
utakaofanyika kwa siku tatu Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 11
Septemba, 2015.
Mkutano
huo ambao utahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, utafunguliwa rasmi na Mfalme wa Lesotho
Letsie III ambaye ni Kiongozi wa kuhamasisha Lishe na Chakula Bora wa
Umoja wa Afrika.
Mkutano
huo ambao ni wa kwanza kufanyika, utajadili masuala mbalimbali
yanayohusu umuhimu wa kuongeza virutubisho kwenye chakula ikiwemo
vitamini na madini muhimu ili kuwawezesha watu duniani kote kuwa na
afya bora kwa ajili ya uzalishaji na kuleta maendeleo na hatimaye
kuondokana na umaskini.
Pia
Mkutano huu ni sehemu ya jitihada za kimataifa katika kukomesha lishe
duni na utapiamlo uliokithiri katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo
Tanzania.
Aidha,
Mkutano huo utawashirikisha wadau na wataalam mbalimbali kutoka
Mashirika ya Kimataifa, Sekta Binafsi na Serikalini. Mashirika hayo ni
pamoja na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la
Afya Duniani (WHO), Shirika la Chakula Duniani (WFP) na Umoja wa Afrika
(AU).
Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) ya Uingereza.
|
No comments:
Post a Comment