Mkurugenzi
Mtendaji 8020 Fashion na Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation
Shamim Mwasha Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha Wanawake Kuwa
Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na
Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake Kufanya
biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini Mada Mbalimbali zilizokuwa Zikijadiliwa.
Mafunzo
ya Ujasiriamali kwa Mwanamke wa Kitanzania kwa Kutumia Vipodozi vya
LuvTouch Manjano yanaendelea.Mradi huo ulianzishwa kuwejengea Uwezo
wanawake Kwenye Ujasiriamali yakisimamiwa na Taasisi ya Manjano
Foundation.
Lengo
la Mradi huo ni kuona kwamba wanwake hawa wanajisimamia na kujikita
vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara
zao kwa lengo la kumuongezea ajira mwanamama na kuondoa dhana za
ukosefu wa ajira kuwa chungu ya yeye kujiwezesha katika kujikimu
mahitaji yake ya msingi, yaani aweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi
kwa kupitia ujasiriamali.
Pamoja
na mafunzo ya biashara, washiriki hawa watanufaika na utaalamu
(Proffessional Makeup Artist).Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo
imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo
zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea ugumu wa kipato na
ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha
yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake,
Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha
wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
Mradi huu Uzinduliwa mwezi Mei mwaka huu na Mama Tunu Pinda.
Mafunzo
haya yametolewa kwa zaidi ya Wanawake 30 ambapo wengi wao tayari
wameshaanza kunuafaika na kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano ambapo
wamewezeshwa
Washiriki hao wakiwa kwenye Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment