Sunday, September 13, 2015

SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAKUWA NI YA VIWANDA-MAGUFULI

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt Magufuli akiwasalimia maelfu ya Wananchi waliofika katika uwanja wa Barafu mjini Igunga,Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akisisitiza mbele ya maelfu ya Wakazi wa mji wa Igunga jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara kuwa Serikali ya awamu ya tano itajenga viwanda mbalimbali vikiwamo viwanda vya nguo ikiwa ni mkakati wa kuinua zao la pamba ambalo linalimwa kwa wingi mikoa ya kanda ziwa,amesema kuwa Serikali yake imedhamiria kuleta mabadiliko bora na si bora mabadiliko na kuongeza kazi kubwa atakayofanya ni kusimamia vema rasilimali za nchi kwa maslahi ya Watanzania wote.
 Dkt Magufuli kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara akiwa katika wilaya ya Maswa na kisha jimbo la Kishapu na Igunga, Dk.Magufuli amesema kuwa anatambua umuhimu wa kuwa na viwanda nchini na hivyo serikali yake itasimamia ujenzi wa viwanda kwa lengo la kuimarisha uchumi na wakati huo huo kusaidia wakulima na wafugaji kunufaika na shughuli wanaofanya nchini.   

  Dk Magufuli akizungumza na wananchi wakati akijinadi  mjini Malampaka, Maswa, ambapo alisema akishinda urais ataanzisha viwanda vingi ili kuongeza thamani ya mazao nchini.
 Dk Magufuli akihutubia wananchi katika Mji wa Maganzo mkoani Shinyanga, ambapo aliomba kumpigia kura ali ashinde awasaidie kuboresha sekta ya uchimbaji madini kwa serikali kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo  kwa kuwapatia mitaji  na vifaa. 


 Wakazi wa Maganzo wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John pombe Magufuli alipokuwa akipita kuelekea Igunga mkoani Tabora kwenye mkutano wa hadhara
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli (katikati) akishangiliwa na wananchi wenye ujumbe wa kumuunga mkono  huku akiwa na mfano wa msumeno wa kuwakatia wezi na mafisadi  akishinda urais wakati wa mkutano wa kampeni  mjini Igunga , Tabora jioni ya leo.
 Wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mjini Maswa

 Wakazi wa Kishapu wakishangilia jambo mara baada ya Mgombea Urais wa CCM kuwahutubia wananchi hao mapema leo mchaa.
  Wananchi wa Kishapu wakimsikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli alipokuwa akijinadi na kuelezea jinsi serikali ya CCM itakavyoboresha sekta mbalimbali nchini
 Sehemu ya umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM wilayani Igunga leo
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Barafu mjini Igunga jioni ya leo,kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mkoani Tabora. 
 Mgombea wa Urais wa CCM Dkt Magufuli akiondoka kwenye uwanja wa Barafu mjini Igunga jioni ya leo mara baada ya kuwahutubia wananchi hao. 

No comments: