wananchi wa Mafinga mjini wakimpokea mwenyekiti wa chama cha CCM mkoa wa Iringa jana mjini mafinga |
MATUKIO KATIKA PICHA (picha: Baraka Nyagenda)
wananchi wa jimbo la Mafinga wakifurahia mkutano
mjumbe wa NEC Marcelina Mkini akimnadi mgombea ubunge Bw Chumi
Waliokuwa wanacham wa CHADEMA wakikabidhiwa kadi za chama cha mapinduzi CCM na mwenyekiti wa chama hicho mkoa baada ya kujiunga na cha cha CCM jana mjini Mafinga. |
MGOMBEA ubunge jimbo la Mafinga Mjini kwa
tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Cosato Chumi juzi amezindua kampeni zake
za kuwania kiti hicho akiwataka watanzania kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa
kumtosa aliyekuwa rafiki yake wa jirani, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward
Lowassa.
Baada ya kutoswa na CCM, Lowassa alikimbilia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na akateuliwa kuwa mgombea wake
urais ambaye pia anawakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) katika kinyang’anyiro hicho.
Akimpigia debe mgombea urais kwa tiketi
ya CCM, Dk John Magufuli, Katibu wa CCM wa wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama amemfananisha
mgombea huyo wa Ukawa na nyuki wa mashineni ambao kwa kawaida huwa hawana uwezo
wa kung’ata.
Chumi aliyesindikizwa na wagombea wa
Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa na Mufindi Kusini, Mendrad Kigola
katika uzinduzi huo, alisema kama Rais Kikwete angekuwa hamfahamu vizuri
Lowassa huenda angemuunga mkono katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani
ya CCM.
“Rais Kikwete aliamua kumtosa Lowassa
kwasababu hakutaka kutuachia mtu mwenye matatizo na mpiga “deal”, kwahiyo
kufahamiana naye kumekuwa na faida kubwa kwa watanzania,” Chumi alisema.
Akiomba kura kwa mamia ya wananchi
waliofurika katika uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa Mashuja mjini
Mafinga, Chumi aliyeshika tochi kubwa muda wake wote aliokuwa akiongea, alisema
anataka kuwa mbunge wa jimbo hilo ili akawamulike na kuwafichua wazembe wanaochelewesha
au kuhujumu kwa makusudi huduma katika sekta mbalimbali jimboni humo.
Akitaja vipaumbele vyake endapo wananchi
wa jimbo hilo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao, alisema atahakikisha katika
kipindi cha miaka mitano ijayo jimbo hilo linakuwa na huduma bora ya maji,
afya, miundombinu na elimu.
Alizitaja sekta zingine atakazozitupia
jicho kuwa ni pamoja na ya biashara na ulinzi na usalama kwa kuhamasisha ujenzi
wa vituo vidogo vya Polisi katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Kwa upande wake, Mgimwa ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii alisema; “Majimbo yote wilaya ya Mufindi
yamepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.”
“Tulikuwa hatuna lami mjini, leo tuna
barabara zenye lami na tumeanza ujenzi wa barabara ya Mgololo kwa kiwango cha
lami. Tumejenga kilomita tatu na tumepata fedha kwa ajili ya kujenga kilometa
nane mwaka huu wa fedha,” alisema.
Katika sekta ya afya na fedha, alisema wodi
ya kisasa ya wazazi imejengwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi ili
kuboresha huduma kwa wajawazito huku huduma za benki zkiongezeka kutoka benki
moja hadi tatu, ambazo ni Mucoba, NMB na Crdb.
Wengine waliohudhuria kampeni hizo ni
pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu aliyezungumzia
Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mahamudu
Madenge aliyeponda kipaumbele cha Lowassa, cha elimu, kwamba kinamsuta jimboni
kwake Monduli.
No comments:
Post a Comment