Monday, August 3, 2015

WAENDESHA BODABODA WASAJILIWA KWA MFUMO MAALUMU

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Alternative Communication Bw. Emmanuel John katika picha ya pamoja na baadhi ya waendesha bodaboda mara baada ya kusajiliwa na kukabidhiwa jezi jana kwenye ukumbu wa Princess Sinza Mapambano, Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Vodacom Stratton Mchau akizungumza na waendesha bodaboda ktk hafla hiyo.
Waendesha boda boda wa Kanda ya Temeke wakiwa katika mkutano mkutano wa pande nne, ambao ni uongozi wa Alternative Communication, Jeshi la Polisi, Vodacom na Bodaboda wenyewe.
Baadhi ya waendesha bodaboda waliokwisha jisajili katika mradi huo wakiwa kazini kuliendeleza libeneke huku wakiwa na uhakika wa bima pale inapotokea ajali.

ZOEZI la kuwatambua waendesha bodaboda na kuwasajili katika mfumo maalumu wa kumbukumbu (database) liliendelea tena mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo safari hii waendesha bodaboda katika kanda ya Kijitonyama wamesajili na kupewa mafunzo muhimu katika maeneo ya usalama barabarani, ujasiriamali na bima.

Kufanyika kwa zoezi hilo hapo jana ni mwendelezo wa mchakato unaofanywa na kampuni ya mawasiliano, masoko na matangazo ya Alternative Communication ya jijini Dar es Salaam, ikishirikiana na jeshi la polisi, lengo likiwa kuwasaidia waendesha bodaboda na abiria wanaotumia usafiri huo kutambulika kwa urahisi inapotokea wamehusika katika matukio ya kihalifu.

Hatua hiyo ina kuja kufuatia madai kuwa baadhi yawaendesha bodaboda wasio kuwa waaminifu hujihusisha katika matukio ya kihalifu au kutumiwa na wahalifu kuvunja Amani na kupotea bila ya kutambulika.

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Emmanuel John Rutagonya, amesema jijini Dar es Salaam kwamba tayari kampuni hiyo imekwisha wasajili bodaboda 3,000 katika mfumo huo. Ameongeza kwamba wale waliosajiliwa pia watapata faida ya kupewa huduma ya bima ya afya, mafunzo ya usalama barabarani na  Ujasiriamali.

Mwenyekiti huyo mtendaji alisema wale wanaosajili wa katika mfumo huo wanapewa koti (Reflectors) zilizo na namba ya usajili kifuani na nyuma ya koti. Namba hiyo ni utambulisho kamili wa mwendesha pikipiki, pia kwenye kofia zao (helmet) itabandikwa namba ya simu ya Kiongozi wa Chama cha Waendesha Bodaboda husika.

“Mtu yoyote akiipiga namba ya chama cha waendesha bodaboda na akataja namba ya usajili wa dereva wa bodaboda, mfumo utamtambua dereva huyo mara moja.”Alisema.

Kwa upande wake Meneja Mauzo Kanda ya Kawe wa Kampuni ya Simu ya Vodacom, ambao ni wadhamini wa mradi huu, Stratton Mchau, alisema Vodacom imeridhishwa sana na mradi huu, na kwamba mbali na mambo mengine ya kiudhamini, Vodacom pia itawateua baadhi ya madereva wa bodaboda kuwa mabalozi wa bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kubwa ya simu nchini.

Waendesha boda boda wa Kanda ya Temeke wakiwa katika mkutano mkutano wa pande nne, ambao ni uongozi wa Alternative Communication, Jeshi la Polisi, Vodacom na Bodaboda wenyewe.

No comments: