Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (kulia) akipatiwa maelezo ya chakula bora kwa wakina mama wakati wakati wa sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika leo kwenye kijiji cha Nkwenda Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
BI. Selina Mussa akionesha namna bora ya kumnyonyesha mtoto wake Brighton Anderson (miezi mitano) kama moja ya kutoa elimu kwa wakina mama waliofika kwenye sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika leo kwenye kijiji cha Nkwenda Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya small boys kutoka kijiji cha Nhinhi Chamwino Adson Amos akipokea zawadi ya Jezi kutoka kwa mgeni rasmi baada ya timu yake kuibuka mshindi kwenye mashindano ya uzinduzi wa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa yaliyofanyika leo kwenye kijiji cha Nkwenda Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge akiwasilisha hotuba ya uzinduzi wa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa yaliyofanyika leo kwenye kijiji cha Nkwenda Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye afya bora walionyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kuchanganyiwa chakula kingine hadi walipofikisha umri wa miezi sita wakati wa sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika leo kwenye kijiji cha Nkwenda Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nkwenda wakiserebuka nyimbo za uhamasishaji wakati wa sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika leo kwenye kijiji cha Nkwenda Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za Uzinduzi wa maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa uliofanyika leo kwenye kijiji cha Nkwenda Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment