Na MatukiodaimaBlog
CHAMA Cha mapinduzi ( CCM) mkoa wa Iringa kimefuta matokeo ya kata tatu za jimbo la Kilolo matokeo yaliyokuwa yakimpa ushindi mkubwa mbunge anaemaliza muda wake Prof Peter Msola na kuagiza uchaguzi huo kurudiwa kesho
Matokeo hayo ambayo yamekataliwa na wagombea wote yanadaiwa kupachikwa katika vituo vya kata hizo tatu japo hata hivyo hayana uhalisia ukilinganisha na idadi ya wanachama wa maeneo husika .
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga alisema kuwa kutokana na dosari mbali mbali ambazo zilijitokeza katika kata hiyo ambazo ni Nyalumbu , Lugalo na Uhambingeto alisema kilichoonyeshwa ni matokeo hayo kuwa tofauti na matokeo halisi ambayo mawakala wa wagombea walikuwa nayo na katika kata hiyo makatibu matawi na kata wa CCM hahakuweza kupeleka matokeo kwa wakati kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi hadi alipoyafuata na kuona kasoro hiyo .
Katibu huyo alisema karatasi zilizoonyesha ushindi wa mgombea mmoja Prof Msolla zilikuwa ni tofauti na karatasi halisi zilizotolewa na chama hivyo kutokana na utofauti huo wagombea wengine waliweza kugomea matokeo hayo .
Hata hivyo mgombea Francis Mkokwa alisema kuwa walishangazwa kuona ghafla mbunge Prof Msola akiongoza katika vituo vya kata hizo ambazo hata matokeo Yake hayakusainiwa na mawakala wa wagombea wengine na ndizo kata ambazo matokeo Yake yalikuwa na utata na wakati wa kampeni mbunge huyo alikuwa hakubaliki katika maeneo ya kata hizo .
Kwani walisema kimsingi matokeo halali ya kata zaidi ya 21 Mwamoto ndie alikuwa akiongoza kwa kura nyingi zaidi kuliko za mgombea mwingine yeyote huku mbunge anaemaliza muda wake akimfukuza kwa mbali na ajabu kushangazwa kuona udanganyifu mkubwa katika kura hizo.
Bila kutaja matokeo hayo alisema walitegemea matokeo ya jumla Mshindi kuwa Mwamoto ila ilitaka kuwa tofauti kwa ambae hakuongoza ktk vituo kutaka kuongoza kwa matokeo ya jumla hivyo kulazimika kuchunguza matokeo hayo na kubaini Wizi huo .
Kwani katika vituo idadi ya kura ni nyingi kuliko ile ya wanachama na wakazi wa eneo husika hata kama wana kijiji wote hadi watoto wa mwaka mmoja wangepiga kura bado kura zilikuwa nyingi kuliko wakazi wa eneo husika kuwa kosa walilolifanya ni kuongeza idadi ya kura za mbunge Prof Msola bila kufuta idadi ya kura za Mwamoto ama idadi ya wapiga kura ya jumla
"ukitazama idadi halisi ya wapiga kura ,kura zilizopigwa na kura zilizoharibika bado ni vitu viwili tofauti na kufananisha Wizi huo ni sawa na Wizi bila mahesabu ....lazima chama kuchukua hatua kali kwa katibu wa chama wilaya na wote waliohusika "
.Mgombea huyo alisema mbali ya kuwa yeye ni mgombea bado kwa sasa wameamua kuungana kupinga wizi huo na kuona mshindi wa kweli anapatikana na sio udanganyifu huo ambao umefanyika.
Kwa upande wake mgombea Ashrafu Chusi pia alisema katika kata hizo kumefanyika udanganyifu mkubwa na kuwa kuna mazingira ya rushwa yalifanyika usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura kwa eneo hilo la mji wa Ilula lenye shida kubwa ya maji watu kupewa rushwa na huduma ya maji kwa kufungulia bomba za maji kwa kituo kimoja baada ya kingine na katika vituo hivyo inasemekana walikuwa wakigawa pia kanga na pesa na pale mbinu hiyo inapobainika walikuwa wakifunga maji kituo husika na kufungua kituo cha pili.
Bw Chusi alisema jambo hilo wanaomba vyombo husika kuweza kuchunguza zaidi ili kuwachukulia hatua wahusika na kuwa hana shaka hata kidogo kuwa mshindi wao katika mchakato alikuwa ni Mwamoto.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Nyalumbu Bw Bruan Mbululo alisema kuwa kimsingi wao walikamilisha kazi yao kwa kwenda kukabidhi matokeo kwa katibu wa CCM wilaya ya Kilolo na kama kuna dalili za udanganyifu wao hawahusiki japo alisema katika kata yake Prof Msola alishinda ila hakumbuki ni kwa kura ngapi.
Kamanda wa taasisi ya kuzuia na kuopambana na rushwa mkoa wa Iringa Yunith Mmari akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema kuwa wanaendelea kuchunguza mchakato huo wa kura za maoni katika kata hizo tatu za jimbo la Kilolo.
No comments:
Post a Comment