Wednesday, August 19, 2015

PROSPER MBENA APOKELEWA NA MAMIA YA WANANCHI JIMBO LA MOROGORO KUSINI

Na John Nditi
MAMIA ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata mbalimbali za Tarafa ya Matombo Mvuha na Bwakila , wilayani Morogoro, wamejitokeza kwa wingi kumlaki mgombea mteule wa chama hicho nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena na udhamini katika fomu za ubunge za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). 
Mgombea Ubunge huyo kupitia CCM, alipokelewa na wanachama na wananchi wa kawaida mpakani wa Jimbo hilo, darajani Ruvu na kusindikishwa na pikipiki umbali wa kilometa 20 hadi eneo la makao makuu wa Kata ya Kisemu, Mtamba . 
 Kabla ya kudhaminiwa na wanachama wa Kata za Tarafa ya Matombo, Augosti 18, mwaka huu, Mbena ambaye pia ni Katibu wa Rais, alitumia fursa hiyo kuwashukuru wanaCCM kwa kumwamini na kupigia kura nyingi zilizomwezesha kuongoza akiwa miongoni mwa wagombea sita wa Jimbo hilo. 
 Alisema kutokana na wanachama kumwamini , amewaomba kuendelea kuunganisha nguvu zao kwa kuwashirikisha mashabiki wa chama hicho kuweza kuwapingia wagombea wa CCM katika nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais siku ya Oktoba 25, mwaka huu. 
 “ Tayari Chama kimewapata wateule wake kwa upande wa Udiwani, Ubunge na Urais...sasa si wakati wa kuendeleza makundi bali kuyavunja na kuunganisha nguvu tuwe timu moja ya ushindi wa CCM” alisema Mbena akiwa katika Ofisi ya Kata ya Kisemu. 
 Alisema, matatizo mengi ya Jimbo hilo anayafahamu kwa vile yenye ni mzaliwa na mkazi wa Jimbo hilo , na aliyataja machache kuwa ni barabara za pembezoni kutopitika na suala la maji, ajira kwa vijana na nyinginezo.
 “ Nina mipango mingi ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa wananchi wa Jimbo hili na nitayasema wakati wa kampeni za uchaguzi...kwani leo nimekuja kwenu kuomba kupata udhamini wa fomu za ubunge za Tume ...hatujaanza kampeni , nitasema wakati huo” alisema Mbena. 
 Akiwa Tarafa ya Mvuha na Bwakila kwa ajili ya kupata udhamini huo, aliwatakawanachama wamwamini na kampeni zitakapoanza rasmi wamchangue awe mbunge wao na kwamba moja na jukumu atakalolisimamia ni kukabiliana na migogoro baina ya wakulima na wafugaji ili wananchi waweze kufanya kazi za uzalishaji mali. 
 Alisema , ni budi wafugaji na wakulima waishi kwa kuaminiana kila mmoja amheshimu mwezake na kwamba dhuruma inapotendeka haki inakosekana . 
 “ Kila upande unamhitaji mwezake mkulima anamhitaji mfugaji na mfugaji anamhitaji mkulima , tusipo heshimiana ndiyo dhuruma ipokuwa na kwa maana hiyo mbunge hawezi kutetea dhuruma , lazima haki ndiyo itawale “ alisema Mbena. 
 Baadhi ya wananchi wa Jimbo hilo, Iddi Selemani pamoja na Michael Pius, kwa nyakati tofauti walisema, wamemchagua Mbena kwa kura nyingi za maoni ndani ya chama wakitambua uwezo wake atakapokuwa mbunge kuweza kusimamia maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo. 
 Naye Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Morogoro Vijijiji , Salum Jaza, akizungumza kabla ya kukaribidha mbunge mteule wa chama katika Jimbo hilo, alisema , wananchi wana matarajio yao ya kupata maendeleo na moja ni kuwezesha kuwa na chuo cha ufundi stadi (VETA) ili kuwawezesha wanafunzi wanaohitimu darasa la saba na sekondari za kata wapate ujuzi wa ufundi wa aina mbalimbali ili wajiajiri wenyewe. . 
Alisema , matatizo mengi ya jimbo hilo yanafahamika na hivyo atakapotapa ridhaa ya kuwa mbunge , ni wajibu kuyapatoia ufumbuzi kwa kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo.
 Mamia ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka  Kata mbalimbali za Tarafa ya Matombo , wilayani Morogoro, wakimlaki mgombea mteule wa chama hicho katika nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena ,( aliyeshika bahasha ) alipowasili Augosti 18,2015  eneo la Mtamba ,  Kata ya Kisemu, tarafa ya Matombo kwa ajili ya kupata wadhamini kwenye  fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

 Mgombea mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena ( kushoto) ,akimwelekeza mwanachama wa chama hicho, Mariselina Joseph , mkazi wa Kata ya Kisemu, tarafa ya Matombo, wilaya ya Morogoro namna ya kujaza fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya udhanini wake , Augosti 18, 2015, Mbena ni Katibu  wa Rais.
 Mgombea mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena ( kushoto) ,akimwelekeza mwanachama wa chama hicho, Mariselina Joseph , mkazi wa Kata ya Kisemu, tarafa ya Matombo, wilaya ya Morogoro namna ya kujaza fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya udhanini wake 
 Katika hatua nyingine, mgombea mteule wa chama hicho  nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini, Mbena  leo ( Augosti 19) amerudisha fomu hizo katika Ofisi ya Msimamzi wa Jimbo baada ya kukamilisha kwa kupata wadhamini wapatao 31 kutoka Kata za Tarafa ya Matombo, Mvuha na Bwakila.

Pongezi kwa Prosper Mbena

No comments: