Balozi
wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, akitoa hotuba yake
wakati wa maonyesho ya sayansi kwa wanafunzi wa sekondari yanayoandaliwa
na shirika la YST ambayo pia Ubalozi wake unadhamini kila mwaka.
Na Daniel Mbega
UBALOZI
wa Ireland nchini Tanzania, umewapatia scholarship Watanzania 14 ili
kusoma kozi mbalimbali za shahada ya uzamili (masters) na huku wanne
kati yao wakienda kusoma vyuo vya nje ya nchi hasa University College
Dublin, Dublin Institute of Technology na National University of Ireland
Maynooth.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Ireland nchini, scholarship hizo
zimetolewa na ubalozi huo kama sehemu ya Mpango wa Mafunzo wa Kila Mwaka
(Fellowship Training Programme), ambapo wataalamu wanne waliobahatika
kwenda ng’ambo watakwenda kusomea kozi za Maendeleo Endelevu
(Sustainable Development), Kilimo na Maisha ya Vijijini (Agriculture and
Rural Livelihoods), Rasilimali Watu (Human Resource Management), na
Immunolojia na Afya ya Binadamu (Immunology and Human Health).
Watanzania wengine 10 wamedhaminiwa kusomea kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya hapa nchini.
Taarifa
hiyo inasema, sherehe za kuwapokea wale walihitimu na kuwakabidhi
scholarship wale wanaokwenda kuanza, zitafanyika kesho mchana katika
ofisi za Ubalozi zilizoko Masaki, jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa
Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan, ndiye atakayetoa scholarship hizo.
Mpango
huo wa Mafunzo wa kila Mwaka, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa kiasi
kikubwa unahusisha Mfuko wa Misaada wa Ireland (Irish Aid) kupitia
program ya maendeleo ya Ubalozi huo nchini Tanzania.
Wanufaika
wa mpango huo wameteuliwa na washirika wa maendeleo wa Ireland nchini
Tanzania, zikiwemo wizara mbalimbali za Serikali, halmashauri za wilaya
na mashirika yasiyo ya kiserikali, ambayo shughuli zao zinawiana na
maeneo ya vipaumbele vya Irish Aid, hususan Kilimo, Afya, Lishe na
Utawala.
Aidha,
wanufaika wote ni watendaji wa kati ambao baada ya kuhitimu masomo yao
watarejea kwenye mashirika na taasisi zao kutumia ujuzi walioupata kwa
manufaa ya jamii.
“Kwa
wanufaika watakaokwenda kusoma nchini Ireland, program inatoa fursa
nzuri ya kujifunza katika hadhi ya kimataifa na kunufaika na hazina
kubwa ya nyenzo za tafiti zinazotolewa kwenye Vyuo Vikuu na Taasisi za
Teknolojia za Ireland,” imeeleza taarifa hiyo.
Ikaongeza:
“Inatarajiwa kwamba mafunzo ya wataalamu hawa yatachangia kwa kiasi
kikubwa maendeleo ya Tanzania, na kuendelea kuimarisha ushirika wa
kielimu baina ya Ireland na Tanzania.”
Ireland,
kupitia Mfuko wa Misaada (Irish Aid), imekuwa ikidhamini Mpango huo wa
Mafunzo nchini Tanzania kwa miaka 40 sasa ambapo program hiyo imekuwa
msingi wa msaada katika kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea na inaendana
na mkakati wa kupunguza umaskini wa nchi washirika wa Ireland, hasa
lengo likiwa kuwapatia wataalamu elimu ya juu ili waendeleze taasisi
zao.
Baadhi
ya taasisi washirika zitakazonufaika na mpango wa mwaka huu ni pamoja
na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Maendeleo
ya Uvuvi, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya
Misenyi, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya
Muheza, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Taasisi ya Chakula na
Lishe, Hospitali ya CCBRT, shirika la Sikika, Mpango wa Maendeleo wa
Kinapa (Kinnapa Development Programme), shirika la CARE Tanzania na
Taasisi ya Afya Ifakara (IHI).
(Imeandaliwa na www.brotherdanny.com/Simu: 0656-331974)
HII HAPA NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
PRESS RELEASE
Fellowship Training Programme Awards Four Scholarships to Study in Ireland
Four
Tanzanian professionals have been awarded scholarships to pursue their
post-graduate masters’ degrees in Ireland. The scholarships were awarded
by the Embassy of Ireland in Tanzania as part an annual Fellowship
Training Programme. The fellows will study Sustainable Development,
Agriculture and Rural Livelihoods, Human Resource Management, and
Immunology and Human Health. A further ten Tanzanians have also been
awarded scholarships to study in Tanzania.
The Fellowship Training Programme is closely connected with Irish Aid, the Embassy’s
development programme in Tanzania. The fellows have been nominated by
Ireland’s development partners in Tanzania, including Government
ministries, district councils and non-governmental organisations, whose
work is closely aligned with Irish Aid’s priority areas - Agriculture,
Health, Nutrition and Governance.
The fellows are all mid-career professionals who, on completion of their studies, are committed to resuming
work with their organisations and putting their acquired specialist
knowledge and skills into practice for the benefit of the wider
community. For the fellows studying in Ireland, the programme presents a
unique opportunity to study in an international setting and benefit
from the research facilities provided at Ireland’s Universities and
Institutes of Technology.
It
is anticipated that the training and development of these key
individuals will contribute to Tanzania’s development, and continue to
strengthen the educational linkages between Ireland and Tanzania.
Notes to the Editor
· * Ireland
has supported a Fellowship Training Programme for 40 years. The
programme is a key element in support of capacity building in developing
countries and is closely aligned with the poverty reduction strategies
of Ireland’s partner countries. The objective is to strengthen capacity of partner organisations through the provision of higher education opportunities.
· * Irish
Aid is the Irish Government’s programme of overseas development. Irish
Aid has been providing development assistance to Tanzania since 1975.
· * Partner organisations benefiting from this year’s fellowship training programme include the Ministry of Agriculture, the Ministry of Livestock and Fisheries Development, Kigoma District Council, Muheza District Council, Ngorongoro District Council, Kondoa District Council, Missenyi District Council, Tanzania Food and Nutrition Centre, CCBRT, Sikika, Kinnapa Development Programme, CARE Tanzania and the Ifakara Health Institute.
· * The
four fellows who will study in Ireland will attend University College
Dublin, Dublin Institute of Technology and the National University of
Ireland Maynooth respectively.
Embassy of Ireland
20th August, 2015
For further information please contact:
Brian Nolan, Second Secretary, Embassy of Ireland, Dar es Salaam
Tel: (+255 22) 260 2355 │ Fax: (+255 22) 260 2362 │ Email: brian.nolan@dfa.ie
No comments:
Post a Comment