Na Teresia Mhagama
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili inayotekelezwa pembeni ya bomba kubwa la gesi katika mkoa wa Mtwara.
Pamoja na kukagua miradi hiyo inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na shirika la Umeme nchini (TANESCO), Naibu Waziri pia amekagua maendeleo ya kituo cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba katika mkoa wa Mtwara.
Katika ziara hiyo Mwijage ameagiza kuwa vifaa vya umeme vinavyohitajika katika utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme, viwasilishwe ndani ya wakati uliopangwa ili miradi hiyo itekelezwe kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ( mwenye suti ya bluu, kulia) akiangalia zoezi la uwekaji nguzo za umeme katika kijiji cha Sinde B, mkoani MTWARA wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ( mwenye suti ya bluu, kulia) akiangalia zoezi la uwekaji nguzo za umeme katika kijiji cha Sinde B, mkoani MTWARA wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya bluu ) akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO) walioko katika kituo cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara mara alipowasili kituoni hapo kukagua mitambo ya kuchakata gesi.Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Kapuulya Musomba .
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kushoto) akimsikiliza mwananchi wa kijiji cha Mnaweni mkoani Mtwara, Bakari Oga ambaye alikuwa akimweleza Naibu Waziri kuhusu changamoto ya
utekelezaji wa miradi ya umeme kijijini hapo.
Baadhi ya mitambo ya kuchakata gesi katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara. Gesi asilia itasafishwa katika kituo hicho kabla ya kusafirisha kwa bomba la Gesi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tano kushoto mstari wa mbele ) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO) walioko katika kituo cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally na kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Tanesco, mkoa wa Mtwara, Daniel Kyando na (aliyevaa kizibao cha rangi ya machungwa) ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Kapuulya Musomba .
Naibu waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini mkoani Mtwara.Kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Mtwara, ALfred Luanda.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika kijiji cha Msanga Mkuu mkoani Mtwara, akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Naibu waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa pili) kushoto akijadiliana jambo na wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini alioambatana nao katika ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa wa Mtwara.Kutoka kushoto ni Mjiolojia Mkuu, Sebastian Shana, Eng. Robert Dulle na Eng. Christopher Bitesigirwe.
No comments:
Post a Comment