Balozi wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing (katikati) akipata maelekezo kuhusu bidhaa za Huawei wakati wa mkutano wa watanzania waishio uhaibuni (Tanzania Diaspora).Kushoto ni Afisa mahusianao na habari,Jimmy na kulia ni Meneja wa bidhaa na huduma wa Huawei hapa nchini, Joseph Lyimo Huawei walikua ni wazamini wakuu wa mkutano huo ulifanyika jijini Dar es salaam katika hoteli ya Serena Augost 14 mwaka huu.
Dr.Lu Youqing lieleza kuwa sasa hivi China na Tanzania wana ushirikiano mzuri ambapo China imekuwa ikisaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuwawezesha watanzania waliopo nchini China.
Mbali na hayo wamekuwa wakisaidia Tanzania kwa njia nyingi moja wapo kwa makampuni ya nchi yao kuwekeza nchini Tanzania.
Huawei ni moja ya kampuni hizo ambapo ina wafanyakazi wengi watanzania na imekuwa ikisaidia watanzania katika mambo mengi ya kielimu na kiteknolojia na kupelekea kukuza uchumi wa tanzania.
Balozi wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing akiwa kakatika picha ya pamoja na mameneja wa Huawei,wa kwanza kutoka kushoto ni Jane Wang Jin afisa masoko wa Huawei na wa pili kutoka kushoto ni Mr.Jimmy Afisa mahusiana na mawasiliano akifuatiwa na mama Mulamula. Wengine ni wafanyakazi wa Huawei Tanzania. Hii ilikua katika mkutano wa watanzania waishio ughaibuni (Diaspora).
Huawei Tanzania walikua moja ya wadhamini wa kongamano hili la siku mbili ambapo kampuni ya Huawei walionyesha jinsi Kamera za CCTV zinavyofanya kazi katika lango kuu la kuingilia katika kongamano hilo ambapo kamera hizo zilionyesha vyema jinsi ya kumwona mtu ambaye anaweza kufanya uharifu wowote mahali pale.
Pia Huawei walikuwa na redio za 4G ambazo walikuwa wakizionyesha katika mabanda kabla na baada ya wanatanzania waishio ughaibuni kuingia na kutoka kujionea vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete,akiwapongeza kampuni ya Huawei kwa kuwapatia cheti cha kudhamini kongamano la watanzania waishio ughaibuni ambapo kampuni ya huawei iliwakilishwa na Meneja wa Huawei hapa nchini, Jimy Jinglio.
China imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania na imetoa kipaumbele kwakufadhili kongamano la wanaDiaspora nje ya nchi kwa kuwapatia elimu na vitu vingine.
Mbali na Hapo China imewekeza mambo mbalimbali nchini Tanzania hasa katika Elimu na Teknologia.
Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe akipewa maelekezo na Mhandisi wa teknologia wa kampuni ya Huawei hapa nchini,Lameck Mangu mara baada ya kutembelea banda la maonyesho la HUWAWEI. HUWAWEI wakiwa na moja ya kampuni zilizodhamini mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe amwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizingumza na watanzania waishio Ughaibuni,(Diaspora) kuhusiana na watanzania hao kuwekeza hapa nchini na kupenda kwao katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) wa wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Rosemary Jain ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo za bongo freva,Peter Msechu akiwaongoza watanzania waishio Ughaibuni maarufu kama Diaspora kuimba wimbo wa Taifa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Watanzania waishio ughaibuni maarufu kama Diaspora wakisikiliza watoa maada hawapo pichania katika mkutano uliowakutanisha uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja wa sheria wa mamlaka ya uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro, Julius akaibebe akiwaasa watanzania waishio ughaibuni kuwekeza hapa nchini hasa katika buga za wanyama ili kuchangia uchumi wa nchi hapa nchini aliyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni(Diaspora) uliofanyika jana na leo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Choice Coffee.co.tld, Rose Swai akizungumza na wanadiaspora waishio ughaibuni kuwekeza kwenye viwanda vinavyotengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutengeneza vifaa vya kuhifadhia(Packeging product) vitu mbalimbali kwa wajasiliamali hapa nchini ili waweze kupata masoko kwa urahisi aliyasema hayo katika kutano uluiwakutanisha watazania waishio ughaibuni uliofanyika katika hoteli ya serene jijini Dar es Salaam.
Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernad Membe akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) mara baada ya mapumziko ya mkutano uliowakutanisha watanzania hao ulifanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
(Picha na Avila Kakingo Globu ya Jamii)
(Picha na Avila Kakingo Globu ya Jamii)
No comments:
Post a Comment