WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, (anayeshughulikia masuala ya Muungano), Samia sSuluhu Hassan,(wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi, (wakwanza kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Property International Ltd, (PIL), Abdulkarim Haleem, (watatu kulia), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Gabriel Silayo, (wane kulia), wakiwa wamekamata mwamvuli ikiwa ni ishara ya umoja, kwenye uzinduzi wa mpango wa kukopesha viwanja wanachama wa PSPF ambapo TPB itaratibu ukopeshwaji huo kwa kutoa fedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Jumanne Agosti 18, 2015.
Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano), Samia Suluhu Hassan, akitoa hotuba.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Gabriel Silayo, akitoa hotuba yake
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake
Msanii wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa PSPF, akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mh. Samia Suluhu Hassa, akimpongeza Silayo baada ya kutoa hotuba yake. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi,(kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa PIL, Abdulkarim Haleem.
NA K-VIS MEDIA
MFUKO wa wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania, TPB, na Taasisi ya Property International Ltd leo Agosti 18, 2015 wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wa mfuko huo katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Hyatt Regency.
Lengo la mkopo huu wa viwanja ili kuwawezesha wanachama wa mfuko huu kumiliki viwanja vilivyopimwa na vilivyo halali kwa mujibu wa taratibu za nchi. Nia ni kwenda sambamba na dira ya PSPF ambayo ni kutoa huduma bora zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wateja wa PSPF, na pia kuitikia mwito wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),walioagiza Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kutoa mafao kwa fomula iliyo sawa kwa watumishi wote.
Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora wa huduma na vivutio vingine kwa wananchama na wananchama watarajiwa.
Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora wa huduma na vivutio vingine kwa wananchama na wananchama watarajiwa.
Ni dhahiri kuwa kila Mtanzania anahitaji kuwa na makazi bora ya kudumu, hivyo mpango huu unaozinduliwa leo hii ni mpango mzuri sana hasa kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kutoa fedha taslimu.
Utaratibuu huu wa kuwakopesha utawanufaisha wengi na hatimaye kufikia kauli mbiu ya Serekali yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.
Utaratibuu huu wa kuwakopesha utawanufaisha wengi na hatimaye kufikia kauli mbiu ya Serekali yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.
Mfuko wa Penshini wa PSPF umeendeleza ushirikiano wake mzuri na Benki ya Posta Tanzania, ambapo kama mnavyofahamu ushirikiano wao ulianzia kwenye utoaji wa Mikopo kwa Wastaafu, Mkopo wa Elimu na Mkopo wa kuanzia Maisha kwa wanachama wapya.
Jitihada hizi zote ni katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonesha imani kwa Benki ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Jitihada hizi zote ni katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonesha imani kwa Benki ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Wanachama wa PSPF waliochangia Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita wanasifa zote za kuweza kukopa viwanja hivi, na watapaswa kulipa ndani ya miaka mitatu. Wanachama walio katika mpango wa Uchangiaji wa Hiari pia watafaidika na mkopo huu. Wanachama wote wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF wanakaribishwa sana kupata mkopo huu maalum kwa ajili yao.
Mgeni Rasmi, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF.
Mgeni rasmi, Samia, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPB.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PIL.
Moshingi, (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa PIL Zohra Moore, (kulia)
Mh. Samia, (kulia), akisindikizwa na Silayo, wakati akiondoka ukumbi wa Hotel ya Hyatt, baada ya hafla hiyo.
Moshingi (kulia), akisalimiana na Mh. Samia Suluhu Hassan, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment