Tuesday, July 14, 2015

SIMU TV: HABARI TOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Mgombea uraisi kupitia CCM pamoja na Mgombea mwenza waahaidi kusimamia rasilimali na kupambana na kero zinazowakabili wananchi. http://youtu.be/7p6ONGZar1A 
Jeshi la polisi Mkoani Mwanza linamshikilia mfanya biashara maarufu mkoani humo kwa tuhuma za kuwapiga risasi watu 2 na kuwaua. http://youtu.be/DpxuQIk1FGE 
Tume ya haki za binadamu na utawala bora imelaani mauaji ya askari polisi na raia katika kituo cha polisi jijini Dar es salaam huku ikitaka wananchi kushirikiana na polisi. http://youtu.be/OZx7jfPf_Dw
Wananchi katika wilaya ya Iringa vijijini wanakabiliwa na upungufu wa chakula huku wakitegemea cha msaada pekee.http://youtu.be/FgHqlB7rl8Y 
Viongozi wa kidini na wanasiasa nchini watakiwa kunyanyua sauti zao kumea dhuluma na kuwatetea wanyonge .http://youtu.be/PK4TbDh86HI 
Baadhi ya wananchi wa jiji la Dar es salaam walitaka jeshi la polisi kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake lifanyie kazi taarifa za kiintelijensi zinazoendelea. http://youtu.be/4DmG4J7yGmQ
 STAR TV NEWS
Zoezi la Kumsaka mgombea Uraisi kupitia Ukawa laendelea huku kukielezwa uwepo wa mvutano mkali baina ya pande hizo.http://youtu.be/cBDkMEaSXJc
 Baadhi ya wananchi nchini waonyesha wasiwasi juu ya uaminifu na utendaji ndani ya jeshi la polisi kufuatia kuvamiwa kwa vituo vya polisi na uporaji silaha. http://youtu.be/XJidFGth0c0
 Watanzania waaswa kuliombea taifa amani,upendo na mshikamano na kujiepusha viashiria vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. http://youtu.be/hvTav8NVewY
 Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia Mfanyabiashara maarufu jijijni humo kwa tuhuma za kuwapiga risasi watu 2 na kuwaua. http://youtu.be/7TGc29QKUyA
 TBC NEWS
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa asema kuna haja kubwa ya viongozi na wadau wa rasiliamali ya maji kukutana na kujadili njia bora za kuunusuru mto Ruaha kufuatia maji yam to huo kupungua kwa kiasi kikubwa. http://youtu.be/Dhd0CTFXro8
 Kiongozi wa dhebu la Shia nchini awaasa viongozi wa siasa kuweka maslahi ya taifa mbele ili kuenzi amani iliyopo nchini.http://simu.tv/LuM5B05
 Wakati waislamu duniani wakijiandaa kusheherekea siku kuu ya Eid-El Fitri waumini wa Kiislamu Tanga wawaasa waislamu kote nchini kuendelea kutenda mema hata baada ya mwezi Mtukufu. http://youtu.be/WXSh5aY5hFg
 Katibu tawala mkoa wa Kigoma atoa agizo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma kutoa eneo kwa ajili ya mradi wa kuandaa mbegu bora za miche ya michikichi. http://youtu.be/cYm679CzRg8
 Mkurugenzi wa TBC ateuliwa kuwa kaimu raisi wa taasisi ya utangazi kusini mwa Afrika SABA. http://youtu.be/iuoprEdDfY4
 AZAM TV NEWS
 Mkutano wa UKAWA waelezwa kufunikwa na kiza kufuatia mivutano ya hapa na pale huku mwenyekiti wa CUF akiripotiwa kutohudhuria kikao. http://youtu.be/mpgSd0YP1lY
 Mgombea mteule wa CCM Dr.John Magufuli atangaza kiama na watendaji wazembe katika serikali wakati akitambulishwa Dar es salaam. http://youtu.be/fUgjlYYtbwg
 Kikao cha UKAWA chaelezwa kukumbwa na changamoto ya mgawanyiko huku CUF wakisusia kikao hicho.http://youtu.be/RzL1rZY7dxc
 Wajasiriamali wadogo waomba sekta za kifedha kutoa mikopo nafuu ili waweze kuendesha biashara zao kukuza mitaji.http://youtu.be/9yw-xNyEsTI
 Wananchi wa wilaya ya Chato waonyesha imani yao juu ya Dr.Magufuli huku wakionyesha imani juu ya uchapa kazi wake.http://youtu.be/uROh4CmhV3I

No comments: