Uwezo wa Misheni ya
Ulinzi wa Amani katika Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO) wa
kutekeleza mamlaka yake kikamilifu utategemea zaidi ushirikiano na uhusiwano wake na mamlaka
za nchi hiyo.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa katika DRC, Bw. Martin Kobler wakati alipowasilisha taarifa yake
mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu
la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya jumaane.
Taarifa Bw. Kobler
kwa Baraza hilo ilihusu maeneo matatu
ambayo ni uchaguzi mkuu utaotarajiwa
kufanyika mwakani, hali ya
usalama na mkakati wa upunguzaji wa idadi ya walinzi wa Amani.
“
Mafanikio ya utekelezaji wa mamlaka yetu
unategemea na kuendelea kwa majadiliano
na ushirikiano na serikali na hususanu kuhusu hali
ya usalama katika eneo la Mashariki na
Mchakato wa Uchaguzi.
Akielezea zaidi kuhusu hali ya usalama,
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, ameliambia
Baraza kwamba, kuna matumaini
katika baadhi ya maeneo.
Akibainisha juu ya operesheni
zinazoendelea dhidi ya kundi la
wanamgambo la Force
de Resistance Patriotique en Ituri ( FPRI) na zinazofanywa na
Jeshi la DRC ( FARDC) kwa kusaidiwa na MONUSCO.
“
Wakati kipaumbele ni kuhakikisha kuwa kundi
hili linasalimisha silaha kwa
hiari, matumizi ya nguvu ilibidi
yafanyike baada ya kunvujwa mara tatu
muda wa mwisho ambao kundi hilo
lilipashwa kusalimisha silaha
zake kwa hiari” amesema Bw. Kobler
Kuhusu operesheni ya pamoja
dhidi ya kundi la Force Democratique de
Liberation du Rwanda ( FDLR) katika
maeneo ya Kivu Magharibu, Kivu ya Kusini na Katanda amsema operesheni hiyo imesimama kwa zaidi ya miezi mitano.
Amefafanua kuwa kusimama kwa
operesheni hiyo ambayo ilitakiwa
ifanywe na FARDC kwa kusaidiwa na
MONUSCO licha ya kwamba pamoja na mambo mengine kulitoka na hoja ya
awali kuhusu haki za binadamu
bali sasa limekwenda mbali zaidi ya hapo.
Akaongeza kwamba wakati MONUSCO ikirejea na kufanya tathmini kuhusu
haki za binadamu ilikuwa inatafuta njia ya namna ya kuendeleza ushirikiano
kupitia mpango uliopo sasa.
Akielezea zaidi kuhusu hali ya
usalama, Bw. Martin Kobler amesisitiza
kuwa wakati serikali ya DRC imepiga hatua kubwa katika kurejesha hali ya Amani katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Bado
wananchi wa eneo la Mashariki ya
nchi hiyo maisha yao yanategemea sana huruma ya makundi ya wanamgambo
wenye silaha.
Pamoja na
mafanikio ya kupunguza
nguvu ya FDLR katika baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyakalia, jeshi la DRC
limejikuta katika mazingira magumu
ya kuyadhibiti na kuyashikilia maeneo yaliyokombolewa na
kwamba hakuna muda wa kusubiri.
Kuhusu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba
mwaka 2016, Bw. Kobler amesema wajibu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi huo
unakuwa wa huru, haki na wazi ni wa serikali yenyewe ya DRC
Akaongeza kwamba tajio
la haraka katika kuhakikisha
kwamba uchaguzi utafanyika kwa wakati ni fedha , kalenda sahihi ya uchaguzi,
uboreshaji wa daftari la wapiga kura na utoaji wa fursa kwa vyama vya upinzani. Akamsifu Rais Kabila kwa kupanua wigo wa majadiliano
na wadau mbalimbali katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.
Katika hatua nyingine. Mwakilishi wa Jordan na ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwanzo dhidi ya DRC, Dina Kawar ,
ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kumkamata na kisha
kukubali kumpeleka nchini Uganda kiongozi wa Kundi la Allied Democratic Force ( ADF) Bw. Jamil
Mukulu
Ametoa shukrani hizo wakati
naye alipokuwa akiwasilisha taarifa ya
Kamati yake mbele ya Baraza Kuu
la Usalama la Umoja wa Mataifa
No comments:
Post a Comment