Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Saada Mkuya Salum akizungumza katika siku ya pili ya mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu ufadhili wa maendeleo ( FFD3) unaoendelea jijini Addis Ababa- Ethiopia
Na Mwandishi
Maalum,
New York
Mkutano wa tatu wa
kimataifa kuhusu ufadhili wa maendeleo,
( FFD3) jana (jumanne) umeingia siku yake
pili ambapo Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Saada Mkuya
Salum alielezea matumaini ya Tanzania
juu ya matokeo ya mkutano huo katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo
endelevu.
Waziri wa Fedha ambaye anamwakilishi Mhe. Rais Jayaka Mrisho Kikwete katika mkutano
huo, amesema kuwa, Tanzania
inaamini kwamba ufadhili wa maendeleo ni moja ya ajenda muhimu kwa Bara
la Afrika . Kwa sababu hiyo Tanzania, inategemea
kuona ufadhili huo unakuwa
na matokeo makubwa katika
kuondoa umaskini katika nchi nyingi za
Afrika.
“ Kama kweli
tunataka kuwa na utekelezaji wa uhakika wa malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015,
Matumaini ya nchi yangu ni kuona kuwa
mkutano huu unatoka na matarajio
mathubuti yatakayo hakikisha mtiririko usio shaka wa rasilimali kuchagiza maendeleo”. Amesema
Mhe.Waziri
Ametoa wito wakuwapo kwa mikakati ya
pamoja baina ya pande zote, kule zitokako au asili ya
raslimali hizo na nchi zinazopokea misaada hiyo lengo likiwa kudhibiti
mrititiko wa fedha chafu, uwezeshwaji wa kukomboa raslimali na
kuzirejesha raslimali hizo kwa nchi husika.
“ Afrika inapoteza karibu
dola bilioni 50 kwa mwaka
kutokana na mtiririko wa fedha chafu
kutoka nchi zinazoendelea, hali
inayosababisha kusababisha uhaba mkubwa
wa hazina ya fedha za kigeni, kupungua kwa makusanyo ya kodi, kufutwa
vyanzo vya uwekezaji uwekezaji na hatimaye kuongezeka kwa umaskini”.
Amesema Waziri wa Fedha.
Kiongozi huyo wa ujumbe wa
Tanzania katika mkutano huo, ameelezea
umuhimu wa Mkakati wa Addis Ababa kujielekeza na kuwa mfumo
madhubuti utakaoimarisha ushirikiano katika masuala ya kodi.
Vile vile Waziri wa fedha, amesisitiza kwamba takwimu zitakazotumiwa na
Taasisi ambazo zitapewa jukumu la kufuatilia na kufanya marejeo kuhusu ufadhili wa maendeleo , takwimu hizo ni lazime zitoke
katika taasisi za takwimu ambazo
zinatambuliwa na serikali ya nchi husika.
Akabinisha
kwamba matumizi ya takwimu
rasmi kutoka taasisi
zinazotambuliwa na serikali , kutaepusha
kutumiwa kwa takwimu ambazo si rasmi na hivyo kusababisha
sitofahamu na migongano kati ya
Nchi wanachama na Umoja wa
Mataifa.
Waziri Saada Mkuya Salumu akatoa wito wa kuongezwa raslimali fedha hususani kwa nchi zinazoendelea ili ziwe na uwezo wa kuboresha mifumo yake ya
ukusanyaji wa takwimu, kuzichambua na kuzifanyia tathmini.
No comments:
Post a Comment