Sunday, July 12, 2015

MAANDAMANO YA AMANI YA WADAU WA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YAFANYIKA LEO JIJINI DAR

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IMEELEZWA kuwa nchi zilizoendelea ndio zinaongoza katika uharibifu wa mazingira kwa utumiaji wa Nuklia ,pamoja na uchimbaji wa Chuma hivyo zinawajibu kuwekeza katika mabadiliko tabia nchi kutokana na kuchangia hali hiyo .

Hayo ameyasema leo Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga wakati wa matembezi ya amani ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi yaliyofanyika  viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Amesema mabadiliko ya tabia ya nchi yamezidi kukua kwa kasi kutokana na uharibuifu wa mzingira unaofanywa na binadamu kwa shughuli za kila siku  huku jitihada za kukabili mabadiliko hayo zikichukua asilimia ndogo.

Mwanga amesema malengo 17 ya maendeleo endelevu ya tabia ya nchi  ya mwaka 2015 -2030  kunahitaji viongozi kushughulikia katika vyanzo mbalimbali vya fedha katika kuweza kufikia malengo na  kushindwa kufanya hivyo kutakuwa na madhara ya ukame,njaa, vifo pamoja na mafuriko.

Aidha amesema kuna mikutano mbalimbali inakuja hivyo ni kila mtu kwa nafasi yake ashiriki katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi iweze kuwa na uchumi imara.

 Wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegeme wakihamasisha urtunzaji wa mazingira katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee ya jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango mbalimbali yenye jumbe tofautitofauti ili kuhamasisha yamii kuachana na uchafuzi wa mazingira ili kuokoa maisha ya watanzania kutokana na kuwa na majamba mbalimbali yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia  ya nchi, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee wakiimba wimbo unaohamasisha utunzaji wa mazingira ili kuepukana na uchafunzi wa mazingira kwa njia mbalimbali, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga akizungumza na wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia  ya nchi mara baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja ya wadau mbalimbali wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa na mabango ambayo yanahamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na ujumbe wa kuokoa maisha ya jamii kwa kutunza mazingira, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments: