Saturday, July 11, 2015

CHAMA CHA WANAWAKE WANASHERIA TANZANIA(TAWLA) WAFUTURU NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA MWANA VINGUNGUTI JIJINI DAR.

 Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam wakiwa wamekaa katika kituo hicho mara baada ya Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),kuwatembelea na kufuturu pamoja nao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wanachama wa  Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) wakichukua Futari kwaajili ya kuwagawia watoto wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam jana. 


Mfanyakazi wa Wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),akiwawekea Futari kwaajili ya kufutari pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo vingunguti jijini Dra es Salaam jana.
 Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini wakifutari pamoja na wanachama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) walipo futuru pamoja na watoto hao katika kituo cha Mwana jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage akiwashukuru wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),walipoamua kutembelea kituo cha mwana.
Mwakilishi wa  Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA), Stella Manongi(wa kwanza kushoto) akizungumza na watoto wa kituo cha Mwana (hawapo pichani) mara baada ya kufutari na watoto hao.
Pia wanachama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA), walitoa msaada wa vitu pamoja na fedha tasilimu na baadi ya vyakula ambavyo vitawasaidia watototo hao kwa siku zijazo kama inavyoonekana wakivitoa vitu hivyo kwenye gari.
Mwakilishi wa chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) akimkabidhi vitu mbalimbali Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage, Mara baada ya Kufutari pamoja na watoto hao.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments: