Monday, July 6, 2015

DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIDIPLOMASIA LA UTEKELEZAJI WA ITIFAKI YA RASIMU YA ARIPO INAYOLENGA KULINDA AINA MBALIMBALI MPYA ZA MIMEA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo Julai 6, 2015.
'WAGOMBEA WANAPOKUTANA', Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni mmoja kati ya wagombea wa Urais kupitia CCM, akizungumza jambo na mgombea mwenzake, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo Julai 6, 2015.
Waziri Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kufungua Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal wakati akihutubia.
Meza Kuu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya kufungua rasmi, leo jijini Arusha.
'WAGOMBEA WANAPOKUTANA' Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni mmoja kati ya wagombea wa Urais kupitia CCM, akifurahia jambo na mgombea mwenzake, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipokuwa akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa ARIPO, Otafiire Kahindi. Picha na OMR.

No comments: