Na Nasibu Mgosso
Awali ya yote nichukue fursa hii kuomba radhi
kwa makosa ya kiuandishi yaliyo jitokeza katika makala iliyopita ambayo
mwanzoni mwa paragrafu ya kwanza nilianza kueleza moto nikitugani, lakini katika maelezo kulitokea mkanganyiko, Sehemu hiyo ilipaswa isomeke hivi:
Moto
ni mgongano endelevu wa kikemikali ambao huzaa joto na mwanga. Mgongano
huo endelevu utasababisha muwako ambao
utaendelea kukua endapo
utapata vitu vikuu vitatu
ambavyo ni joto, hewa
ya oksijeni na kuni(vitu
vinavyoungua). Vituhivyo kitaalam
tunaviita ’fire element’.
Oksijeni
nimiongoni mwa vitu vinavyo saidio moto kuwaka haizalishwi na moto kamailivyo someka katika
makala iliyo pita.
Baada
ya marekebisho hayo sasa tuendelee
na kinga na taadhari dhidi ya moto.
Kunavyanzo
vingi vya moto lakini chanzo kikubwa
ni sisi
Binadamu kwa sababu ya asili na alakati za maisha ya kila
siku kuhusisha matumizi ya moto kwa maana ya mwako, nishati ya umeme pamoja na vyombo vya usafiri
na usafirishaji. Katika mahitaji hayo
inatulazimu kujenga urafiki na moto bila kujali hatari iliyopo.
Aina
ubishi kwamba moto ni nyenzo muhimu katika
maisha yetu ya kila siku, na
niadui yetu mkubwa sana anaye penda kutu
shambulia akitokea ndani ya jengo au
chombo .
Kutokana na mbinu hiyo , moto umekuwa ukisababisha ualibifu wa mali, ulemavu, pamoja na vifo kila siku iendayo kwa mungu.
Hatuwezi
kuepuka isitokee kabisa lakini tunaweza kupunguza matukio hayo kama tutapata elimu sahihi ya
kinga na taadhali ya moto.
KINGA
NA TAHADHARI KATIKA MAJENGO.
Tuki
zingatia kanuni za ujenzi wa majengo na
kuwatumia wataalamu kwakufuata ushauri wao na kuheshimu taaluma
zao tunaweza kufanikiwa kupunguza majanga ya moto pamoja na majanga mengine.
Nianze
na umeme kama miongoni mwa chanzo cha moto katika maeneo ya mijini japokuwa kwasasa vijijini nako huduma hiyo
imeanza kupatikana. Nivyema kutumia mafundi umeme walio somea na kusajiliwa na
mamlaka husika.
Epuka
kutumia vifaa visivyo na ubora vinavyo
patikana kwa bei ya chini, kumbuka bure
ghali . Matumizi ya vifaa vya umeme
chakavu kama jiko, pasi, jokofu,
Oveni kutoka nje , siyo salama kwasababu
vinakuwa vimechoka hivyo vinaweza kusababisha hitilafu na kusababisha moto.
Matumizi ya vifaa vingi katika chanzo kimoja(extension ) vinaweza
kusababisha moto kutokea , ni vizuri
unap weka mfumo wa umeme katika jengo weka swichi soketi zaidi ya
moja katika kila chumba kulingana na
ukubwa pamoja na mahitaji. Kwa mfano
sehemu ya kupumzikia(seating room ) ni vema ikawa na vyanzo vingi vya
umeme kwa sababu matumizi uwa makubwa ukilinganisha na vyumbani.
Aitha mfumo wa umeme ukaguliwe marakwa mara
kuangalia kama kuna hitilafu, badirisha
waya kila baada ya miaka 15. Hakikisha waya wa ethi hauna tatizo lolote pia shaba inayo chimbiwa aridhini iwe na ukubwa
wa kutosho kulingana na mahitaji ya
jengo.
Kwa
maeneo ya mikoa yenye Radi kwawkiasi
kikubwa, vifaa vya mawasiliano kama minara na setelaiti dishi nivizuri viwe
na mfumo wa ethi wa kujitegemea
kwasababu uwezekano wa kupigwa
na radi
na kusababisha moto nimkubwa zaidi.
Jinsi
ya kutambua kama mfumo wa ethi haufanyi
kazi.
Kama mfumo wa
ethi haufanyi kazi vizuri mambo yafuatayo yatajitokeza, vifaa
vya ndani kama friji vitakuwa na
shoti ukigusa utahisi hali ya kutetemeshwa , jua
kwamba umeme una rudishwa kwenye
soketi bleaka ili upelekwe aridhini kupitia mfumo wa ethi
lakini kwasababu mfumo huo
haufanyi kazi, umeme unakosa muelekeo na kurudi katika mzunguko, ikiwa kuna
sehemu yenye hitilafu moto
utaanzia apo, fanya marekebisho
kabla ajari haijatokea.
Matumizi
ya mishumaa bila ya taadhari ni hatari
sana, imekuwa kawaida kusikia nyumba imeungua chanzo kikiwa mshuma . Kama ni
lazima kutumia mshumaa chukua hatua zifuatazo , chomeka
mshumaa katika mdomo wa chupa sio
plastiki , tumia nguvu kuushindilia,
hakikisha kiasi kisicho pungua nusu
kidole kimezama ndani ya chupa.
Weka mbali na ukuta, pazia, kitanda, viti na vitu
vyote vinavyo weza kuungua. Nihatari
kulala ukiwa umeacha mshumaa unawaka, usiweke vimiminika vinavyo lipuka ndani .
Vyombo kama Pikipiki na jenereta ni
hatari kuhifadhiwa ndani pia mafuta ya
akiba kwamatumizi ya vyombo hivyo yasi hifadhiwe ndani .
Matumizi ya gesi
ya zingatie usalama kulingana na maelekezo ya kitaalamu, watoto wa dogo wasitumie wakiwa pekeyao.
Zima
vifaa vya umeme kama havitumiki au kama hakuna mtu nyumbani. Weka
ving’amuzi vya moshi au joto
katika nyumba yako , kuwa na mitungi ya kuzimia moto ya huduma ya kwanza
hakikisha familia ina jua jinsi ya kuutumia.
Kumbuka
king’amuzi cha joto au moshi hakizimi moto kita piga alam kuashilia tukio, wewe utatakiwa kuzima umeme wa nyumba yote kagua
kujua kama kuna tukio. Ikiwa utabaini moto tumia mtungi
wako kuukabili mapema kabla haujawa mkubwa, fahamu mtungi huo ni wa huduma ya kwanza, hauwezi kuzima moto mkubwa.
Pia
vipo vifaa kama hivyo vinavyo fanya kazi
bila kutegemea uwepo wa mtu, vina ji
ongoza vyenyewe vinatumia mfumo wa
kung’amua joto na likizidi asilimia 68 chupa itapasuka ambapo ita ruhusu
mgandamizo wa hewa yenye mchanganyiko na
dry powder kutoka na kupunguza kiwango
cha okisijeni ili kuzimamoto. Faida za
kifaa hiki ni kubwa kwasababu kitaokoa hatakama nyumbani au ndani ya jengo
hakuna mtu.
Aidha majengo marefu zaidi ya ghorofa 7 yafungwe
mfumo wa kuzima moto wenye kujiongoza
wenyewe unao tumia maji, (automatic sprinkler
system ) na yawe na mabomba yasiyo na maji yaliyo anzia chini ya jengo kwa
nje yatakayo tumiwa na zimamoto
kupandisha maji juu pindi moto unapo tokea.
Sambamba
na yote hayo kumbuka kuomba msada,
pigakelele kuita watu, wasiliana
na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa simu namba 114 eleza hali halisi ya
tukio, eneo husika na jinsi ya kufika hapo.
Angalizo,
114 ni namba ya dharura kwajili ya matukio ya dharura ambayo haya husiani
na uvunjaji wa sheria,
namba hihi inapatikana kwa mitandao yote katika mikoa yote Tanzania Bara, matumizi
mabaya ya namba hihi ni matumizi mabaya ya mitandao, kuwa makini
Fahamu kuwa miongoni mwa sababu zinazo
sababisha Zimamoto kuchelewa katika matukio ni taarifa za matukio zisizo za kweli za mara kwa mara. Inapo tokea kuna tukio la
kweli inachukua muda mrefu kubaini
ukweli huo na hiyo nimoja ya sababu za wao kuchelewa
kufika eneo la tukio.
Tukishirikiana kwapamoja tuta punguza majanga ya moto.
Kwa
maoni , ushauri tuwasiliane kwa
nmgosso@yahoo.com / godfreypeter37@yahoo.com
No comments:
Post a Comment