NA NASIBU MGOSSO.
Awali ya yote nichukue fulsa hii kuomba radhi kwa makosa ya kiuandishi yaliyo jitokeza katika makala iliyopita ambayo mwanzoni mwa paragrafu ya kwanza nilianza kueleza moto nikitugani, lakini katika maelezo kulitokea mkanganyiko, Sehemu hiyo ilipaswa isomeke hivi:
Moto ni mgongano endelevu wa kikemikali ambao uzaa joto na mwanga. Mgongano huo endelevu utasababisha muwako ambao utaendelea kukua endapo utapata vitu vikuu vitatu ambavyo ni joto, hewa ya oksijeni na kuni(vitu vinavyoungua). Vituhivyo kitaalam tunaviita ’fire element’.
Oksijeni nimiongoni mwa vitu vinavyo saidio moto kuwaka haizalishwi na moto kamailivyo someka katika makala iliyo pita.
Baada ya marekebisho hayo sasa tuendelee na kinga na taadhari dhidi ya moto.
Kunavyanzo vingi vya moto lakini chanzo kikubwa ni sisi Binadamu kwa sababu ya asili na alakati za maisha ya kila siku kuhusisha matumizi ya moto kwa maana ya mwako, nishati ya umeme pamoja na vyombo vya usafiri na usafirishaji. Katika mahitaji hayo inatulazimu kujenga urafiki na moto bila kujali hatari iliyopo.
Aina ubishi kwamba moto ni nyenzo muhimu katika maisha yetu ya kila siku, na niadui yetu mkubwa sana anaye penda kutu shambulia akitokea ndani ya jengo au chombo .
Kutokana na mbinu hiyo , moto umekuwa ukisababisha ualibifu wa mali, ulemavu, pamoja na vifo kila siku iendayo kwa mungu.
Hatuwezi kuepuka isitokee kabisa lakini tunaweza kupunguza matukio hayo kama tuta pata elimu sahihi ya kinga na taadhali ya moto.
KINGA NA TAADHARI KATIKA MAJENGO.
Tuki zingatia kanuni za ujenzi wa majengo na kuwatumia wataalamu kwakufuata ushauri wao na kuheshimu taaluma zao tunaweza kufanikiwa kupunguza majanga ya moto pamoja na majanga mengine.
Nianze na umeme kama miongoni mwa chanzo cha moto katika maeneo ya mijini japokuwa kwasasa vijijini nako huduma hiyo imeanza kupatikana. Nivyema kutumia mafundi umeme walio somea na kusajiliwa na mamlaka husika.
Epuka kutumia vifaa visivyo na ubora vinavyo patikana kwa bei ya chini, kumbuka bure ghali . Matumizi ya vifaa vya umeme chakavu kama jiko, pasi, jokofu, Oveni kutoka nje , siyo salama kwasababu vinakuwa vimechoka hivyo vinaweza kusababisha hitilafu na kusababisha moto.
Matumizi ya vifaa vingi katika chanzo kimoja(extension ) vinaweza kusababisha moto kutokea , ni vizuri unapo weka mfumo wa umeme katika jengo weka swichi soketi zaid ya moja katika kila chumba kulingana na ukubwa pamoja na mahitaji. Kwamfano sehemu ya kupumzikia(seating room ) ni vema ikawa na vyanzo vingi vya umeme kwasababu matumizi uwa makubwa ukilinganisha na vyumbani.
Aitha mfumo wa umeme ukaguliwe marakwa mara kuangalia kama kuna hitilafu, badirisha waya kila baada ya miaka 15. Akikisha waya wa ethi hauna tatizo lolote pia shaba inayo chimbiwa aridhini iwe na ukubwa wa kutosho kulingana na mahitaji ya jengo.
Kwa maeneo ya mikoa yenye Radi kwawkiasi kikubwa, vifaa vya mawasiliano kama minara na setelaiti dishi nivizuri viwe na mfumo wa ethi wa kujitegemea kwasababu uwezekano wa kupigwa na radi na kusababisha moto nimkubwa zaidi.
Jinsi ya kutambua kama mfumo wa ethi haufanyi kazi.
Kama mfumo wa ethi haufanyi kazi vizuri mambo yafuatayo yatajitokeza, vifaa vya ndani kama friji vitakuwa na shoti ukigusa utahisi hali ya kutetemeshwa , jua kwamba umeme una rudishwa kwenye soketi bleaka ili upelekwe aridhini kupitia mfumo wa ethi lakini kwasababu mfumo huo haufanyi kazi, umeme unakosa muelekeo na kurudi katika mzunguko, ikiwa kuna sehemu yenye hitilafu moto utaanzia apo, fanya marekebisho kabla ajari haijatokea.
Matumizi ya mishumaa bila ya taadhari ni hatari sana, imekuwa kawaida kusikia nyumba imeungua chanzo kikiwa mshuma . Kama ni lazima kutumia mshumaa chukua hatua zifuatazo , chomeka mshumaa katika mdomo wa chupa sio plastiki , tumia nguvu kuushindilia, hakikisha kiasi kisicho pungua nusu kidole kimezama ndani ya chupa.
Weka mbali na ukuta, pazia, kitanda, viti na vitu vyote vinavyo weza kuungua. Nihatari kulala ukiwa umeacha mshumaa unawaka, usiweke vimiminika vinavyo lipuka ndani . Vyombo kama Pikipiki na jenereta ni hatari kuhifadhiwa ndani pia mafuta ya akiba kwamatumizi ya vyombo hivyo yasi hifadhiwe ndani .
Matumizi ya gesi ya zingatie usalama kulingana na maelekezo ya kitaalamu, watoto wa dogo wasitumie wakiwa pekeyao.
Zima vifaa vya umeme kama havitumiki au kama hakuna mtu nyumbani. Weka ving’amuzi vya moshi au joto katika nyumba yako , kuwa na mitungi ya kuzimia moto ya huduma ya kwanza hakikisha familia ina jua jinsi ya kuutumia.
Kumbuka king’amuzi cha joto au moshi hakizimi moto kita piga alam kuashilia tukio, wewe utatakiwa kuzima umeme wa nyumba yote kagua kujua kama kuna tukio. Ikiwa utabaini moto tumia mtungi wako kuukabili mapema kabla haujawa mkubwa, fahamu mtungi huo ni wa huduma ya kwanza, hauwezi kuzima moto mkubwa.
Pia vipo vifaa kama hivyo vinavyo fanya kazi bila kutegemea uwepo wa mtu, vina ji ongoza vyenyewe vinatumia mfumo wa kung’amua joto na likizidi asilimia 68 chupa itapasuka ambapo ita ruhusu mgandamizo wa hewa yenye mchanganyiko na dry powder kutoka na kupunguza kiwango cha okisijeni ili kuzimamoto. Faida za kifaa hiki ni kubwa kwasababu kitaokoa hatakama nyumbani au ndani ya jengo hakuna mtu.
Aidha majengo marefu zaidi ya ghorofa 7 yafungwe mfumo wa kuzima moto wenye kujiongoza wenyewe unao tumia maji, (automatic sprinkler system ) na yawe na mabomba yasiyo na maji yaliyo anzia chini ya jengo kwa nje yatakayo tumiwa na zimamoto kupandisha maji juu pindi moto unapo tokea.
Sambamba na yote hayo kumbuka kuomba msada, pigakelele kuita watu, wasiliana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa simu namba 114 eleza hali halisi ya tukio, eneo husika na jinsi ya kufika hapo.
Angalizo, 114 ni namba ya dharura kwajili ya matukio ya dharura ambayo haya husiani na uvunjaji wa sheria, namba hihi inapatikana kwa mitandao yote katika mikoa yote Tanzania Bara, matumizi mabaya ya namba hihi ni matumizi mabaya ya mitandao, kuwa makini Fahamu kuwa miongoni mwa sababu zinazo sababisha Zimamoto kuchelewa katika matukio ni taarifa za matukio zisizo za kweli za mara kwa mara.
Inapo tokea kuna tukio la kweli inachukua muda mrefu kubaini ukweli huo na hiyo nimoja ya sababu za wao kuchelewa kufika eneo la tukio.
Tukishirikiana kwapamoja tuta punguza majanga ya moto.
Kwa maoni , ushauri tuwasiliane kwa
nmgosso@yahoo.com / godfreypeter37@yahoo.com
No comments:
Post a Comment