Tuesday, July 21, 2015

Airtel wakabidhi jezi kwa timu zitakazoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars

Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Kinondoni,Isaac Mazwile kwaajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, inayoanza tarehe 24 Julai mkoani Mbeya. katikati ni Afisa Uhusiano Airtel,Jane Matinde. Makabidhiano hayo yalifanyika leo jijini Dar-es-Salaam.
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Ilala Kanuti Daudi kwaajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars katikati ni Afisa Uhusiano Airtel Jane Matinde. Makabidhiano hayo yalifanyika leo jijini Dar-es-Salaam.
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Nyenza akiongea wakati kupokea vifaa vya michezo ya Airtel Rising Stars kutoka kwa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel , Kulia Afisa Uhusiano Airtel,Jane Matinde kushoto ni Afisa Maendeleo wa TFF bwana Jemadari.
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu (katikati kushoto), Afisa Uhusiano Airtel, Jane Matinde, katibu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Kinondoni,Isaac Mazwile kulia na Afisa Maendeleo wa TFF bwana Jemadari kwa pamoja wakionyesha vifaa vya michezo vitakavyotumika wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars. Airtel jana ilikabithi vifaa kwa timu zote zitakazoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu.
Afisa Uhusiano Airtel, Jane Matinde akimkabithi vifaa vya michezo Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Nyenza kwaajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, inayotegemea kutimu vumbi kuanzia Ijumaa, Julai 24, 2015 mkoani Mbeya.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi jezi kwa timu za wasichana na wavulana za U-17 zinazoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza katika ngazi ya mkoa Ijumaa, Julai 24.

Mkoa wa Dar es Salam unajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke huku timu nyingine zikitoka mikoa ya Morogoro, Mbeya, Arusha na Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya soka la Vijana ya TFF Ayoub Nyenzi alisema kwamba maandalizi yote kwa ajili ya michuano hiyo ngazi za mikoa yamekamilika.

“Ni matarajio yetu kuwa tutashuhudia mechi zilizojaa ushindani na mvuto na vilevile ningependa kuona mamlaka zinazohusika na usimamizi wa michuano hiyo ngazi ya mkoa zikichagua wachezaji bora ambao wataunda timu za kombaini za mikoa tayari kwa kushiriki fainali hizo ngazi ya taifa zitazofanyika jijini Dar es Salaam baadaye mwezi Septemba”,alisema.

Mkoa wa Mbeya utakuwa wa kwanza kuzindua mashindano yake Julai 24, ikifuatiwa na mkoa wa Dar es Salaam Julai 27, Morogoro Agusti 1 na Arusha Agusti 9, huku Mwanza wakitarajia kufanya uzinduzi wao mnamo Agusti 15. Wageni rasmi katika hafla za uzinduzi wa mikoa wanatarajiwa kuwa wakuu wa mikoa husika.

Mikoa yote shiriki inatarajiwa kuwa na timu za wavulana na wasichana isipokuwa mkoa wa Arusha ambao unatoa timu ya wasichana pekee na Morogoro inayoshirikisha wavulana tu. Huu ni mwaka wa tano mfululizo ambao michuano hii imekuwa ikifanyika nchini, huku ikichangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa vipaji vyenye manufaa kwa Taifa.

Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde, ameelezea nia ya dhati ya kampuni yake kuendelea kudhamini programu za vijana huku akiomba sapoti kutoka kwa TFF, Wizara inayoshughulikia masuala ya michezo pamoja na wadau wengine wa mchezo wa soka.

Alisema Airtel Rising Stars mwaka huu inaenda bega kwa bega na kampeni mpya ya ‘It’s Now’ huku nahodha wa Ivory Coast ambaye pia ni kiungo wa Manchester City Yaya Toure akiongoza kampeni hiyo. Kampeni hii inalenga kulea na kukuza vipaji barani Afrika kupitia nyanja mbalimbali kama vile michezo, mtindo wa maisha na mziki lakini vilevile kuwapa mbinu zitazaowawezesha kupata ufumbuzi wa masuala ya kiteknolojia na kuona fursa zinazowazunguka.

Airtel Rising Stars ni program ambayo ipo bara zima la Afrika maalum kwa ajili kuwapa vijana fursa ya kuonesha vipaji vyao na kuwarahisishia makocha kupata vijana ambao watawaendeleza vipaji vyao kwa manufaa ya baadaye.

No comments: