Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano
akifungua rasmi warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo
vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU
warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
Gianluca
Azzon Mwakilishi wa EU Nchini Tanzania akiwasilisha mada katika
warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana
na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la
AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo
imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
Tom
Bishop kutoka shirika lisilo la Kiserikali la AMEND akiwasilisha mada
katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo
vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika hilo na
kufadhiliwa na Jumuiya ya umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika
kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia
mada mbalimbali katika warsha hiyo.
Baadhi
ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia
mada mbalimbali katika warsha hiyo.
Kamishina
Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi
cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mkurugenzi wa mtandao wa
Fullshangweblog Bw. John Bukuku.
Kamishina
Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi
cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Kibuda Chalila Mwandishi mwandamizi
wa Michuzi Media.
Kamishina
Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi
cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mwandishi wa habari wa magazeti ya
serikali TSN Bi. Regina Kumba.
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika warsha hiyo
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
IMEELEZWA kuwa suala la usalama barabarani ni ni jukumu la kikosi cha usalama
barabarani hali ambayo jamii imejengeka na utamaduni huo na kusahau suala hilo ni jamii nzima katika mapambano ya kupunguza ajali za barabarani.
Hayo
ameyasema leo Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani,Johansen Kahatano wakati wa mafunzo kwa waandishi habari juu
ya kuhabarisha jamii katika suala la usalama barabarani iliyofadhiliwa
na Umoja wa Ulaya (EU).
Kahatano
amesema kuwa kikosi cha usalama barabarani kimekuwa kikitoa elimu juu
ya usalama barabarani kwa wananchi pamoja na madereva katika kuzingatia
sheria zilizowekwa katika kuondokana na ajali zinazotokana na makosa ya
kibinadamu.
Amesema
jamii ikipata mwamko wa katika kutambua sheria za usalama barabarani
kuna uwezekano wa kuondokana na ajali ambazo zinapoteza watu pamoja na
kuacha watu wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu.
“Kikosi
cha usalama barabani pekee yake hakiwezi ni wakati umefika kwa jamii
kuweka suala hili kwenye vichwa vyao kuwa wanamchango katika wa
kusukuma gurudumu katika kupambana na ajali katika sehemu zao”amesema
Kahatano.
Katika
kuhamasisha masuala ya Usalama Barabarani ,Mwandishi wa Citizeni Mkinga
Mkinga amesema ni wakati umefika kwa waandishi kutambua umuhimu wetu wa
kutoa taarifa za kuelimisha wananchi juu ya usalama barabarani.
Umoja
wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika mradi wa uboreshaji
wa miundombinu katika mashule ili kuweza kuondokana na ajali za
wanafunzi katika maeneo ya karibu na barabara.
No comments:
Post a Comment