Monday, May 18, 2015

Idara ya uratibu wa maafa yaridhishwa na zoezi la upokeaji waomba hifadhi kutoka burundi

Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen. Mbazi Msuya akimpongeza Nahodha wa meli ya Mv. Liemba, Mande Mangapi mara baada ya kuwafikisha salama waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wapatao 600, katika bandari ya Kigoma kutoka Kagunga, saa mbili usiku tarehe 15 Mei 2015, kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoani Kigoma, Salvatory Shauri.
Ujumbe uliongozwa na Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen. Mbazi Msuya ukiwa katika bandari ya Kigoma kwa ajili ya kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwasili kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Baadhi ya waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwasili katika bandari ya Kigoma kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Askari wa Jeshi la Polisi, Konstebo Genovefa Kizinza akifanya ukaguzi wa mzigo aliowasili nao muomba hifadhi ya Ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwasili katika bandari ya Kigoma kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Baadhi ya waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamejipanga tayari kusafirishwa kwa mabasi hadi kwenye kambi ya mpito ya Lake Tanganyika muomba hifadhi ya Ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwasili katika bandari ya Kigoma kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen. Mbazi Msuya (katikati) akiwa na Uongozi wa mkoa na baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayohudumia wakimbizi mara baada ya kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi katika bandari ya Kigoma kutoka Kagunga, saa mbili usiku tarehe 15 Mei 2015, (mwenye tai) ni Kaimu Katibu Tawala mkoani Kigoma, Salvatory Shauri.

No comments: