Monday, May 18, 2015

Balozi Seif Ali Iddi afunga Semina ya Siku Nne ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na watendaji Wakuu wa Serikali

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifunga Semina ya Siku Nne ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na watendaji Wakuu wa Serikali juu ya uchambuzi wa Bajeti na Masuala ya Uchumi iliyokuwa ikifanyika katika ukumbi wa Z. Ocean Hoteli Chuwini Wilaya ya Magharibi “A”.
Baadhi ya Wajumbne wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotub a ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akiifunga semina ya uchamguzi wa Bajeti na masuala yua Uchumi.
Waziri wa Fedha ZanzibarMh. Omar Yussuf kulia na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Nassor Ahmed Mazrui wakiwa makini kufutailia Hotuba ya Balozi Seif kwenye Semina yao.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Serikali ambao wameshiriki Semina ya uchambuzi wa Bajeti na masuala ya Uchumi hapo Z. Ocean Hoteli Chuwini Wilaya ya Magharibi “ A “.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho Kulia na Waziri wa Nchi Ikulu na Utawala Bora Dr. Mwinyihaji Makame wakikamilisha Semina hayo ya uchambuzi wa Bajeti na masuala ya Uchumi. Picha na - OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema  yapo matumaini makubwa ya kukua kwa Uchumi wa Zanzibar  kukua ambako kutategemea pia Uchaguzi Mkuu wa Mwezi wa Oktoba mwaka huu kama utakwenda kwa amani na utulivu.

Alisema Serikali kwa upande wake itahakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar inaendesha Uchaguzi wenye uwazi, huru na haki kwa wagombea wote watakaobahatika kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Balozi Seif Ali Iddi akiwa kiongozi wa shughuli za Serikali alisema hayo wakati akiifunga Semina ya siku Nne ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na watendaji Wakuu wa Serikali juu ya uchambuzi wa Bajeti na Masuala ya Uchumi iliyokuwa ikifanyika katika ukumbi wa Z Ocean Hoteli Chuwini Wilaya ya Magharibi “A”.

Alisema Uchaguzi ulio salama na haki utakuwa kichocheo kikubwa   kitakachotoa fursa ya kusaidia kukua kwa uchumi wa Taifa sambamba na kuhamasiha wawekezaji wengi zaidi kumiminika nchini kwa lengo la kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi.

Balozi Seif aliwanasihi wanasiasa ni vyema wakajiepusha na kauli za kuchochea vurugu, huku akiwataka wananchi kutokubali kuchochewa kuanzisha fujo wakati Waandishi wa Habari wakawajibika ipasavyo kutekeleza majukumu yao kwa jamii katika misingi ya uadilifu.

Akizungumzia  Bajeti inayozingatia matokeo { PBB } ambao ni mfumo mpya utakaotumika katika majadiliano ya Baraza la Wawakilishi kwenye Bajeti ya mwaka huu Balozi Seif alisema mfumo huu utawasaidia Wananchi kuelewa kwa uwazi Bajeti ya Serikali yao na imeleta matokeo gani kwao.

Alisema Mfumo huu mpya ambao utawapa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuendelea kujifunza unasaidia kujenga uwazi katika suala zima la matumizi ya Serikali jambo ambalo ni muhimu katika jitihada za kukuza uchumi wa Wananchi.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/5/2015.

No comments: