Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ambaye ni Mwanamitindo na Mbunifu Mavazi maarufu nchini Tanzania, kwa sasa akifanyia kazi zake nchini Marekani, akizungumza wakati wa semina ya siku moja, iliyowaleta pamoja, wanamitindo "kinda" wa Tanzania, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Jumapili Mei 17, 2015. Semina hiyo ililenga kuwafunza na kubadilishana uzoefu juu ya tasnia hiyo inayokuwa kwa kasi. Semina hiyo ya siku moja, ilitayarishwa kwa pamoja na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na mwanamitindo huyo nguli. Katika maelezo yake, Flaviana, alisema yeye binafsi ni mwanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa hiari yaani "PSPF Supplementary Scheme-kwa kifupi PSS", na kuwataka wanamitindo waliohudhuria semina hiyo, kufuata nyayo zake. Aliwaeleza umuhimu wa wanamitindo hao ambao wengi ni vijana, kujiunga na mpango huo kwa faida yao ya sasa na baadaye, kwani yeye anafaidika sana kuwa mwanachama wa Mfuko huo. Baada ya maelezo hayo yaliyofuatiwa na balozi mwingine wa Mfuko huo, Msanii maarufu wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, naye aliwapa "doze" wanamitindo hao juu ya ukuhimu wa wao kuchangamkia fursa mapema kwani ndio mtindo wa kisasa. Hali kadhalika afisa masoko wa Mfuko huo Magira Werema, aliwahakikishia wanamitindo hao kuwa Mfuko huo ni Mfuko bora na wala hawatajuta waingiapo kuwa wanachama. Baada ya hotuba hizo, wanamitindo hao walizichangamkia fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo amba;po karibu washiriki wote zaidi ya 100 walijiunga na Mfuko huo. |
No comments:
Post a Comment