Ofisa Mtendaji Masoko wa EATV, Brendansia Kileo (kulia)
akifafanua jambo mbele ya wandishi (hawapo pichani), kushoto kwake ni Digital
&Branding Manager wa 361 degree, Hurbert Kissas na kulia ni Meneja wa chapa
wa vinywaji vikali wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija.
Maonyesho ya siku mbili ya Harusi Tanzania maarufu kama
‘Harusi Trade Fair 2015’, yanayotarajiwa kufanyika Machi 13-14 mwaka huu katika
ukumbi wa Danken House, uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Wakiongea na wandishi wa habari mapema jana Machi 2, wakati wa kutambulisha
wadhaamini wakuu wa mwaka huu ambao ni kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kwa
vinywaji vya Baileys ‘Cream with Spirit’ na Johnnie Walker ‘Gold Label’,
wandaaji wa maonyesho hayo kampuni ya 361 degree, kupitia kwa Meneja biashara
na maendeleo, Hamis Omary alisema tayari
maandalizi hayo yamepamba moto huku washiriki zaidi ya 50, wakitarajiwa
kushiriki.
“mwaka huu ni wa sita kwa maonyesho
haya. Hivyo tunajivunia
mafanikio mbalimbali. Tunashukuru wadhamini wetu kampuni ya bia ya
Serengeti kwa kujitokeza kudhamini mwaka huu ni faraja kwetu” alisema
Hamis Omary.
Aidha, aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia
maonyesho hayo kwani ni ya kipekee ambayo yatatoa dira na mwangaza kwa
wanaharusi wanaotarajia kuoa, kuoana ikiwemo kupata uzoefu na mipangilio ya
shughuli yao ambayo kwa kawaida ni tukio la mara moja katika maisha ya binadamu.
“Harusi ni tukio zuri, ambalo hutokea mara moja tu, huku
likiunganisha familia na jamii pamoja, hivyo nia yetu ni kuwapa maharusi
mahitaji yao yoote muhimu kwa pamoja na kwa wakati mmoja, na maonyesho haya
ndio sehemu muafaka kwa hilo” alisema Hamis Omary.
Ambapo alisema kuwa, katika maonyesho hayo wadau wote wa harusi wataonyesha bidhaa
zao ambapo kiingilio ni bure kwa watu wote, ila wakati wa maonyesho ya ubunifu
wa mavazi ya harusi, yatakuwa na kiingilio cha sh 25,000 kwa kila mtu.
Hamis Omary aliwataja baadhi ya wadau hao ni pamoja na watu
wa mapambo (Decorations ), watu wa vyakula (Catering),watu wa matarumbeta, MC,
Watengeneza keki, wapamba maharusi na wengine wengi.
Aidha kwa upande wa baadhi ya makampuni ambao ni wadau wa
bidhaa za harusi ni pamoja na: 101 STUDIOS, AN NISA ABAYAS, MOIZ HUSEIN
STUDIOS, EDNA DESIGN, THE PRINT HOUSE, LOTUS CREATIVE, MANYATA HOUSE OF
ACCESSORIES na wengine wengi.
Huku mbunifu wa mitindo, mkubwa ambaye anatamba pia
kimataifa, Mustafa Hassanali akitarajiwa kuonyesha mavazi ya harusi.
Kwa upande wake, Meneja wa chapa ya vinywaji vikali wa
kampuni ya Serengeti, Shomari Shija alisema bidhaa zao hizo zenye ubora wa
kimataifa, zimekuwa zikipendwa na watu mbalimbali ikiwemo kwenye sherehe hivyo
ni muda muafaka kwa watanzania kuendelea kuwaunga mkono na kufurahia muonekano
mzuri.
“Kinywaji chetu cha Baileys na Johnnie Walker ni miongoni
mwa vinywaji vinavyopendwa sana kwenye harusi mbalimbali. Pia tunaweka chapa ya
majina ya wanaharusi kwenye vinywaji vyetu hivyo ni muda muafaka wa kuendelea
kutuunga mkono” alisema Shija.
Kwa upande wake, Afisa Masoko Mkuu wa kituo cha televisheni
cha EATV, Brendansia Kileo ambao nao ni wadhamini aliwaomba vijana mbalimbali
kuendelea kuwaunga mkono kwani kila siku wanatoa vitu vipya ambavyo vinajenga
na kutengeneza mustakabali wa maisha yao ikiwemo vipindi bora.
Maonyesho hayo ya Harusi Trade Fair 2015, yanaandaliwa na
361 Degree, huku yakidhaminiwa na kinywaji cha Baileys na Johnnie Walker, East
Africa radio/EATV na wengine wengi.
Brand Meneger-Spirit wa Serengeti Breweries Limited, Shomari
Shija(mwenye koti jeusi) akifafanua jambo mbele ya wandishi wa habari hawapo
pichani) wakati wa utambulisho huo.Meneja wa chapa wa vinywaji vikali wa Serengeti Breweries
Limited, Shomari Shija (mwenye koti jeusi) akifafanua jambo mbele ya wandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
Maonyesho haya ya Harusi ambayo hufanyika kila mwaka,
huwaleta pamoja wahusika wote wa mambo ya Harusi katika kujenga na kutengeneza
mtandao wa kimafanikio baina yao, na ndio maana maonyesho haya yamekuwa ni ya
kwanza na ya aina yake Tanzania.
Hivyo ni fursa ya kipekee kwa wenza watarajiwa kujitokeza
kwa wingi kushuhudia namna ya mchakato wa shughuli za harusi zinavyokuwa
mwanzo, kati na mwisho.
Ambapo kwa mwaka huu yatapambwa na vitu kama keki, maua, wapiga
picha, magauni ya Harusi, bila kusahau mengi na yenye ubunifu katika Harusi.
Ambapo pia kwa maharusi, familia, na wale wote wanaohusika
na kamati za Harusi ndio muda muafaka wa kuhudhuria ili kujionea na kujua mengi
yahusuyo Harusi na mahitaji yake.
Kwa maelezo zaidi tembelea hapa. http://harusitradefair.com/
No comments:
Post a Comment