Monday, March 9, 2015

Dkt. Shein akabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani,Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mwakilishi wa VSO Tanzania Jean Van Wetter wakati alipowasili katika viwanja vya Ukimbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo katika hafla ya sherehe ya kukabidhi Vihori kwa wakulima wa Mwani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar Mohamed (wa pili kushoto) na Katibu wa Wizara hiyo Bi Asha Ali Abdalla (kulia)wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo katika hafla ya sherehe ya kukabidhi Vihori kwa wakulima wa Mwani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa kwa kutumia zao la mwani na kikundi cha Ulezi ni Kazi cha shehia ya Fujoni Jimbo la Kitope) wakati wa sherehe za kukabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.
wakinamama wakulima wa mwani kutoka sehemu tofauti za Unguja na Pemba wakiwa katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja katika sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani kwa Mikoa ya Unguja na Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kihori Bi.Zainab Daudi Haji mkulima wa mwani wa Uroa Wilya ya Kati Mkoa wa Kusini wakati wa sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kihori Bw.Kombo Salim Hamadi mkulima wa mwani wa Tumbe Magharibi Kaskazini Pemba wakati wa sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wakati sherehe za kukabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Viongozi,Wananchi na wakulima wa mwani wakiwa katika sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.]

No comments: