Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakitazama Msafara wa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ukikatiza kwenye moja ya
daraja wakati wakielekea katika kijiji hicho cha Mkoka,Wilayani Kongwa
mkoani Dodoma,Ndugu kinana aliweka jiwe la msingi la kitega uchumi cha
tawi la CCM pamoja na kufungua Ofisi ya CCM Tawi la Mkoka
Mamia
ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye
uwanja wa kijiji hicho kumsikiliza Katibu Mkuu waa CCM,Ndugu Kinana na
Ujumbe wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo,wilayani Kongwa
mkoani Dodoma.
Kikundi
cha ngoma ya asili ya Kigogo,kiitwacho KIFARU kitumbuiza katika uwanja
wa kijiji cha Mkoka kabla ya mkutano wa hadhara kuanza.
Mbunge
wa jimbo la Kongwa na Naibu Spika wa Bunge,Mh.Job Ndugai akiwahutubia
wakazi wa kijiji cha Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni
ya leo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Kongwa
mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwaja wa kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye
anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba
na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na
kuyatafutia ufumbuzi.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka wakishangilia jambo wakati
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye
anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba
na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na
kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye wakiwa wamefuatana na wananchi walipokuwa wakiwasili katika
uwanja wa Mkoka kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara,mbali ya Uongozi
huo wa juu wa CCM,pia waliambatana Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job
Ndugai,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Chiku Galawa,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Dodoma,Mh.Addam Kimbisa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.
Baadhi ya akina mama wa kijiji cha Chamae kata ya Hogolo wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake,wilayani Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani juu ya jengo akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai wakishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Njoge,Kata ya Njoge pamoja na kusalimia Wananchi wa eneo hilo.
Jengo la zahanati hiyo ya Kijiji cha Njoge kama lionekavyo kwa nje,ujenzi wake ukiendelea kwa kasi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Njoge,mara baada ya kushiriki ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho,wilayani Kongwa,mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Mh Adam Kimbisa akizungumza mbele ya wanakijiji cha Njoge na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwa ajili ya kuwasalimia na kuzisikiliza kero zao.
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini,wakati alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Njoge,wilayani Kongwa kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa Zahanati ya kijiji na kusikiliza matatizo ya Wananchi hao.
Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kushiriki ujenzi wa dara la shule ya msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa matofali kwa ajili ya darasa la shule ya msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa,anaeshuhudia kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji katika kijiji cha
Mlali Wilayani Kongwa,mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni
mia sita ulianza kujengwa mnamo mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mei
2014,lakini kwa bahati mbaya mradi huo haukukamilika kwa wakati kutokana
na ukosefu wa fedha.Mbunge wa jimbo hilo la Kongwa,Mh.Ndugai alieleza
kuwa mradi huo kwa sasa umekwishakamilika kwa asilimia tisini na kwamba
mradi huo wa maji safi na salama utawanufaisha wanakijiji wapatao mia
saba na zaidi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kushiriki kupalilia shamba la kijiji katika Kata ya Iduo,wilayani Kongwa
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wa pilia shoto akishiriki kupalilia shamba la kijiji la Alizeti katika Kata ya Iduo,wilayani Kongwa,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Mh.Adam Kimbisa.
No comments:
Post a Comment