Friday, March 20, 2015

ENG. STELLA MANYANYA AKAGUA UJENZI WA MRADI WA MAJI SAFI NA MAJI TAKA SUMBAWANGA MJINI

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akipata maelezo ya mradi wa Maji Taka katika Manispaa ya Sumbawanga kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Sumbawanga (SUWASA) Ndugu Zakaria Ngunda alipofika kutembelea mradi huo tarehe 19/03/2015. Ujenzi wa mradi wa Maji Taka umeshakamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni magari matatu kwa ajili ya kuzolea taka za vyooni zitakazomwagwa katika mtambo huo  ili uanze kufanya kazi. Miradi yote mikubwa ya Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga inagharimu zaidi ya fedha za Kitanzania shilingi bilioni 30.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakandarasi wanaojenga mradi Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga ambao ni Techno Fab na Mkandarasi mshauri GKW ambapo amewataka kuongeza kasi kumaliza mradi huo ambao upo nyuma ya wakati. Amemuagiza Mkandarasi anaejenga kukamilisha ujenzi huo kwa kipindi cha miezi miwili ijayo licha ya kuomba kuongezewa muda wa miezi sita ili aweze kukamilisha kazi hiyo. 

Alisema kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ni lazima uende na wakati kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa wakati na hivyo kupisha malalamiko ya wananchi kwa Serikali yao. Kwa upande mwingine ameuagiza uongozi wa Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga kumfikishia taarifa za Mkandarasi Herken Builders Ltd aliyojenga mradi wa maji wa visima nane na "pumps" ambazo hazifanyi kazi aweze kumchukulia hatua stakihi ikiwepo kumuandikia barua kuwa hastahiki kufanya kazi katika Mkoa wake wa Rukwa. 
 Mradi wa Bwawa la kuchujia Maji Taka Mjini Sumbawanga ukiwa umekamilika. 
 Sehemu ya Bwawa hilo.
 Sehemu ya Mradi wa Maji Safi ambao ni Chujio la kuchuja Maji Safi kabla ya kwenda kwa walaji.
 Sehemu ya Mradi wa Maji Safi.
Picha nyuma ni sehemu pia ya ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi unaoendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

No comments: