Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
TATIZO la Vifo vya watoto njiti limezidi kukua kutokana na kukosekana kwa vitendea kazi katika vituo vya kutolea hudum za afya.
Hayo ameyasema, Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo wakati wa kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel ambao utajihusisha katika kusaidia upatikanaji wa vitendea kazi vya hospitali kwa watoto wanaozaliwa njiti iliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.amesema atatoa ushirikiano wa kutosha kwa mfuko huo huku akiutaka uende pia Zanzibar na kukutana Baraza la wawakilishi.
Kombo amesema Mollel amejitambua na ana umuhimu wa kusaidia watoto njiti kutokakana na kutambua alikotokea na matatizo gani wanayokumbana nayo watoto njiti.
Mwenyekiti wa Mfuko huo ,Doris Mollel ambaye Mrembo wa Singida 2014/15,amesema yeye alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2 na kuona kuna umuhimu wa kusaidia watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.
Amesema lengo la mfuko ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia jamii katika upande wa watoto njiti ambapo takwimu zilizopo zinaeleza idadi ni ndogo kutokana na jamii nyingine hazina utamaduni wa kwenda kujifungulia katika vituo vya afya hivyo elimu inahitajika kufanya jamii hizi zifike katika vituo vya afya na kuwezeshwa kwa vituo hivyo kuwa na vifaa na kuweza kupunguza vifo hivi kutoka 9000 hadi 1000 au kuondoa kabisa.
Doris amesema takwimu zinaonyesha kuwa watoto 213,000 wanazaliwa wakiwa njiti na 9,000 wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya vifaa vya kufanya waweze kukua katika joto linalostahili.
Kwa upande wa Balozi Mwanaidi Maajah amesema kuwa Doris amejitoa katika kusaidia upande wake aliotokea kwa kutambua kuwa kuna mchango unahitajika katika kusaidia watoto wanaozaliwa wakiwa njiti.
Katika hafla hiyo watu mbalimbali wamechangia ambapo fedha tasilim sh.800,000 zimepatikana na ahadi ni sh. ya Milioni 4.7.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel akizungumza na wageni waalikwa waliofika kwenye hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel,uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo (pili kushoto),Balozi Mwanaid Maajar (kulia),Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel (katikati) pamoja na wadau wengine wa Mfuko huo wakishiriki kwa pamoja kukata keki,kuashiria uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Doris Mollel,uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo akimpongeza Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel kwa kuona jukumu la kusaidia jamii katika kuokoa maisha ya watoto njiti.
Sehemu ya Wageni waalikwa katika hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliohudhulia hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment