Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu akiwasilisha mada kuhusu "Exchange Rate Developments in Tanzania and Implications for the Economy" kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa Semina fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam tarehe 18 Machi, 2015. Katika mada yake Prof. Ndulu alielezea pamoja na mambo mengine umuhimu wa Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nje ili kudhibiti mfumuko wa bei na kuipandisha thamani Sarafu ya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine hususan Dola ya Marekani, kuimarisha upatikanaji wa fedha za nje kama dola na kuvutia zaidi wawekezaji nchini. |
No comments:
Post a Comment